Shalom.
Katika Agano la kale.
Neno sayuni limetumika mazingira tofauti tofauti, mfano, baada ya Daudi kuiteka Yerusalemu, ile sehemu ilitiwa ngome ya sayuni (2Samweli 5:7), hivyo kwa hapa imetumika Kama mji wa Daudi au wa Mungu.
Kadhalika na mlimani ambapo hekalu la Mungu lilijengwa liliitwa pia mlima sayuni, (Yeremia 31: 6,12)
Mahali pengine utaona ni watu wa Mungu au Israel kwa Agano la kale..
Isaya 60: 14 “Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako [Israeli] na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli”
Katika vitabu kama Maombolezo, Zakaria 9:9, sefania 3:14-19, Israel inaitwa binti sayuni. Kwa Ujumla sayuni ilikuwa ni watu wa Mungu au Israel.
Katika Agano jipya.
Sayuni ni ufalme wa Mungu Katika Ulimwengu wa Roho, hasa kwa Waamini ( waliookolewa).
Waebrania 12: 22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,”
Mtume wa Mungu Paulo anaonesha kuwa Waamini au kanisa wanaishi katika mlima sayuni wa Mungu au katika mji wa Mungu Yerusalemu wa kiroho.
Mtume Petro pia anaonesha hili..
1Petro 2: 6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika SAYUNI JIWE KUU LA PEMBENI, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7 Basi, HESHIMA HII NI KWENU NINYI MNAOAMINI. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo.”
Hivyo basi, katika Agano Bora zaidi la Mungu yaani Agano jipya sayuni au mji wa Mungu Yerusalemu ni kanisa au wale Waliaminio jina la Mwokozi Yesu Kristo. Hivyo nasi pia tuendelee kudumu na kuishi katika Mji mtakatifu wa Mungu au Yerusalemu, Ambayo Mungu ameifanya pale wanapoishi Waaminio pamoja naye kama Roho Mtakatifu.
Amina.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.