Nini maana ya shubaka kibiblia ?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana apewe sifa karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Bwana wetu yesu kristo.

Shubaka ni dirisha lililojengwa kwa kupishanisha vipande vya mbao au chuma au kitu kingine kama pazia katikati ya dirisha Hilo.

Ujenzi wa madirisha hayo haupo kama wa kisasa kwakuwa madirisha ya Sasa yapo wazi sana yaani hauwezi kuona kitu chochote kimekatiza katikati unaweza ukakuta kioo tupu eneo lote lakini madirisha ya zamani hayo ya shubaka ilikuwa ni kawaida kuyakuta karibu katika nyumba zote.

Neno Hilo tunalipata kwenye biblia kama inavyosema.

Mithali 7:23

23 Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.

24 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.

25 Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.

26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.

27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti”.

Hivyo inatukumbusha kuwa Mungu anatutazama kutoka juu mbinguni akiyaangalia matendo yetu na tabia zetu yeye ndiye anayechunguza na kujua Siri za mioyo yetu.Hivyo inatupasa tuzishike Sheria na Amri za Bwana ili tuurithi ufalme wa Mbinguni.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *