Wakrete ni watu gani(Tito 1:12)

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

Swali: tunajifunza habari ya WAKRETE kwamba walikuwa ni WAONGO, na walishuhudiwa na nabii wao!
JE? Walidanganya Nini na ni nani basi huyo nabii wao?

Jibu: WAKRETE ni Jamii ya watu wanaoishi katika visiwa vya krete huko Ugiriki. Mtume Paulo anaandika waraka kwa Tito dhidi ya kanisa na Uongozi katika uteuzi.

Kwa ufupi, tabia mojawapo ya watu wa krete walikuwa ni WAONGO kwa viwango vikubwa! Ambapo mpaka mtu wa kwao ( Nabii wao) wenyewe aliandika kuhusiana na tabia hiyo na nyinginezo kama ulafi na Uvivu.

Biblia haijataja nabii huyo ni nani wala haionyeshi waraka wake lakini tunaona mtume Paulo akiwa anaunukuu..

Tito 1:12 “..MTU WA KWAO, NABII WAO WENYEWE, AMESEMA, WAKRETE NI WAONGO SIKU ZOTE, HAYAWANI WABAYA, WALAFI WAVIVU”

Kihistoria Alikuwepo mwana filosofia wa Krete aliitwa “EPIMEDINES” ambaye alikuwa ni nabii wa Mungu wa kigiriki aliyeitwaa “ZEU” (Matendo 14:12-13)
Lakini pia EPIMEDINES alikuwa ni mtunzi wa mashahiri ya kumtukuza yule Mungu wao; Shairi mojawapo alilolitunga ni lile linalotumiwa na mtume Paulo, linasema hivi..

…“Walikutengenezea kaburi, takatifu, uliye juu (zeu), Wakrete, waongo siku zote, wanyama wabaya, wavivu wa tumbo. Lakini wewe hukufa: unaishi na unakaa milele. Kwa maana ndani yako tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu”…

Shairi hili la kumtukuza ZEU (mungu wao) liliaminika sana na wakrete maana pia walimuamini sawa yule nabii wao EPIMEDINES. Hivyo mtume Paulo kwa maana alilijua Shairi lile ndipo analitumia kama Uthibitisho na msisitizo wa ukweli kuhusu dhambi ya WAKRETE ambayo ni Uongo, lakini si lengo la mtume Paulo kumthibitisha nabii wao! Bali kuthibitisha Uongo wa wakrete ambao ni dhahiri ata kwa wasioamini.
Hivyo ndivyo anamuonya Tito akemee Hilo.

Tunajifunza kuwa Uongo ni Mbaya! Afanyaye Uongo ni mtumwa wa Uongo! Na baba wa Uongo ni Shetani! Hivyo wanaodanganya wote ni watoto wa Ibilisi.
Tusome..

Yohana 8:44 “ Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo”.

Bwana Atusaidie tuushinde UONGO.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *