Nini maana ya Bafe(mwanzo 49:17)

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana wetu Yesu Kristo na Asifiwe sana. 

Habari hizi utazipata katika ule utabiri wa Yakobo juu ya watoto wake, alipokuwa akiwabariki, tunaona anapofikia kwa Dani anasema Dani yeye atakuwa BAFE. Sasa JE? Ni nani huyo BAFE?

Turejee..

Mwanzo 49:17″ Dani atakuwa nyoka barabarani, BAFE katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali.

18 Wokovu wako nimeungoja, Ee Bwana.”

Bafe ni jamii ya nyoka aina ya kifutu. Hivyo yakobo anamwona mwanawe kama nyoka, ambaye maisha yake ni mavumbini

lakini amemng’ata farasi kisigino na kumfanya Ashindwe kuendelea; hii inamfanya hata mpanda farasi naye kuanguka kabla ya kuvipiga vita vyake.

Sikiliza, Yakobo alimaanisha kuwa huenda Dani akadharaulika sana ( wa mavumbini) lakini amebeba wokovu mkubwa juu ya watu wake, pale ambapo kibinadamu wanategemea mpanda farasi ashambuliwe na mikuki na mbinu nyingine kubwa kubwa za kijeshi, lakini yeye Dani atauma kisigino tu, kwa farasi wao na nguvu yao maadui itaisha hapo.

Hii inatufunulia kwamba kila mmoja wetu amepewa karama yake tofauti na mwenzie ili sote tuwe wakamilifu (Waefeso 4:12a), endapo karama hiyo itatumika kwa usahihi itaweza kumweka chini adui. Wengi huthamini zile karama zinazoonekana kuwa na Heshima machoni pao kama Uinjilisti, Ualimu, Uchungaji unabii n.k

Lakini sikiliza Mpendwa, kamwe usidharau karama yako unayoihisi kuwa ni ndogo, kumbuka vile visivyoonekana sikuzote ndivyo huwa na umuhimu mkubwa , mfano watu wanaona miguu, mikono, macho lakini kuna Figo, ini, moyo ambavyo havionekani lakini sote twajua uthamani wake ulivyo.

Pamoja na yote katika baraka zile Yuda aliitwa Simba, Isakari aliitwa punda, Dani aliitwa Bafe lakini wote wakaunda Israel Taifa la Mungu.

Jitathamini mwenyewe; JE! Unaithamini karama yako? Au umeidharau na kutamani za wengine!!

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *