Shalom, karibu tuongeze maarifa..
Sote tunafahamu wingi wa neno mlango ni Milango, kwa kuwa malango na milango ni neno moja linalofanana, Bwana Yesu alilitakamka neno hili,..
Mathayo 16:18 “ Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; WALA MILANGO YA KUZIMU HAITALISHINDA.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.
hiyo mamlaka alikabidhiwa mtume Petro pamoja na mitume wengine, Yohana 20:23
Malango ni sehemu ya maingilio ya watu au vitu, tunaingia ndani ya nyumba au ndani ya mji kupitia Milango yake, kwa kuwa hakuna njia nyingine..
Bwana aliposema neno hili kwamba atalijenga kanisa wala malango ya kuzimu haitalishinda, alimaanisha kanisa ambalo Kristo atalijenga litakuwa ni kanisa lenye nguvu hivyo Milango ya kuzimu halitaweza kushinda..
Je hiyo Milango ya kuzimu ni ipi?
Milango ya kuzimu ni yale mambo yote maovu yanayomfanya mtu awe na sababu zote za yeye kuingia kuzimu,
Tuangalie mambo hayo..
1Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? MSIDANGANYIKE; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi”
Hivyo Mambo yote machafu yasiyompendeza Mungu ni Milango ya kuzimu, wizi ni lango la kwenda kuzimu, kufanya uasherati na uzinzi ni lango la kuzimu, ufisadi ni lango la kuzimu,kuabudu masanamu ni lango la kuzimu, pamoja na mengine mengi, hata ukisema umefanya moja tu bado utaenda kuzimu tu kwa kuwa Milango ya kuzimu ipo mingi, njia yako itakuwa ni hiyo hiyo..
Yakobo 2:10 “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria”.
Na kanisa Bwana atakalolijenga litakuwa ni kanisa lisilo na hila yoyote wala kunyanzi, kwasababu litaendea lango moja tu la Mbinguni, Ni Yesu, wala halitaweza kushikwa na malango ya kuzimu, na ndo kanisa Kristo aliahidi kulitengeneza..
Alilianza kanisa kulijenga siku ya pentecoste, siku Roho Mtakatifu aliposhuka juu ya watu wake, wakajazwa Roho Mtakatifu na kupokea nguvu za kuishinda Milango ya kuzimu..
Kwasababu Roho Mtakatifu ni muhuri wa Mungu, anaposhuka na kukaa ndani ya mtu anaua kiu yote ya kufanya dhambi, mara nyingi hupekea watu kushangaa ni kwa namna gani kijana wa Mungu anaweza kuishi bila kuzini, au kuiba,au kunywa pombe, na huku hatumii nguvu kushinda hizo hali,
Unafikia mahali unajiuliza, anawezaje kuishi bila kuwa na fedha, na ana amani nyingi bila kupelekea kurudi nyuma na kumkana Yesu Kristo, ni nguvu waliyopewa ili kuishinda Milango yote ya kuzimu..
Jiulize umeipokea hii nguvu,
Kwa ufunuo ambao Petro alipewa wa kwamba Yesu atalijenga kanisa wala malango ya kuzimu haitalishinda, UFUNUO HUO NI KUWA YESU NI MWANA WA MUNGU
Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”
Na wewe ukihitaji uishinde Milango yote ya kuzimu, njia ni moja tu, ni KUMWAMINI YESU NDIYE MWANA WA MUNGU, msingi huu ndio kanisa la Yesu litajengwa juu yake, ukitafuta njia nyingine milele hautaweza kuishinda hii Milango ya kuzimu..
Fanya maamuzi ya haraka,kwa kumpokea Bwana Yesu ndani yako kwa kutubu kwa kumaanisha,ukabatiwze ubatizo sahihi ili upokee Roho Mtakatifu ambaye ndiye muhuri wa Mungu, kwasababu yeye ndiye atakayekupa nguvu za kushinda malango yote ya huko kuzimu
Maandiko yanasema kuzimu haishibi soma Mithali 30:16) waoshuka huko ni wengi kila siku na milango yake ni mingi..
Maran atha..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.