Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na libarikiwe.
Turejee jibu kutoka 5:14-16
“Na WANYAPARA wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza?
15 Basi WANYAPARA wa wana wa Israeli wakaenda, wakamlilia Farao, wakisema, Mbona umetutendea hivi, sisi watumwa wako?
16 Watumwa wako hawapewi majani, nao wanatuambia, Fanyeni matofali; na tazama, watumwa wako wapigwa; lakini kosa hilo ni la watu wako mwenyewe”.
Wanyapara ni viongozi au wasimamizi wa watumwa wenzao.
Mfano katika Magereza wale wafungwa wanaoteuliwa kuwa viongozi wa wenzao ndio huitwa Wanyapara. Mkuu wa gereza anapotoa agizo fulani basi yule nyapara ndio huliwasilisha agizo hilo kwa wafungwa wenzie yeye akiwa kama kiongozi.
Kipindi wana wa Israeli wapo utumwani misri wale askari wa farao walichagua baadhi ya wafungwa na kuwafanya wanyapara kwa wale wenzao. Hivyo endapo kungekuwa na tatizo lolote aidha mgomo au ulegevu kwa wale Wana wa Israeli basi waliokuwa wanaathirika kwanza ni Wanyapara, Maana Askari wa farao wangeshughulika kwanza na wale Wanyapara kabla ya watumwa
Kutoka 5:14 “Na wanyapara wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza?”
Dunia ya Leo na Shetani anao nyapara wake aliowaweka chini ya wote wanaotumikishwa na dhambi, maana biblia inasema atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi, hivyo kama ni mtumwa basi atakuwa na nyapara wake.
Kama unaishi chini ya dhambi(Ulevi, uasherati) Basi yule unayeishi nae kama ni mke au mume ni Nyapara wa ibilisi kwako wewe na anakutesa maana wewe ni Mtumwa, basi lazima Shetani akupe Nyapara wa Utumwa wa kazi zake.
Mkatae Leo Shetani na Nyapara wake mkubali Yesu Leo Utoke katika Utumwa na upate Uzima wa milele.
Ubarikiwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.