Ifahamu maana ya yakobo 3:1 ndugu zangu msiwe waalimu wengi.

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tujifunze biblia..


Yakobo 3:1
“Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.”

Ukipeleka katika lugha ya kiingereza ” Not many of you should become teachers ..” au unaweza kusema ” pasiwepo na waalimu wengi kati yenu”


Roho Mtakatifu anamvuvia yakobo kuyasema haya yanayolitafuna sana kanisa, Hii huonekana pindi Kila mtu anapokuwa ni mjuaji au kukosa utaratibu, jambo baya sana kwa kanisa. Sababu kanisa huongozwa na karama za Roho, yaani waalimu, nabii,wainjilisti n.k


Jambo hili linapotokea kanisani Kila mtu ni mwalimu au mchungaji kinachozaliwa ni pepo la machafuko, sababu unakuta mtu ni mfasiri lugha lakini anataka afundishe au achunge, madhara ni kuongeza au kupunguza neno la Mungu kwasababu madhara yake ni makubwa ukiachana na adhabu yake ni kubwa na ipo tayari kwa wayafanyao hayo..


Ufunuo wa Yohana 22:18-19
18 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”

Kwa neno hili ndugutunakumbushwa na kututaadharisha Kila mmoja kukaa katika nafasi yake kama ni mwalimu, Mfasiri, mtoaji, mchungaji , si vinginevyo, yaani unakuta wewe n mwalimu na unataka ufanye na wewe Uimbaji, hakika tunatafuta hukumu

Amen .

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *