dini ya chrislam ni ipi? na je tunaruhisiwa kuiamini?

Maswali ya Biblia No Comments

Chrislam ina tambulika kama ni muungamaniko wa maneno makuu mawili. (Yaani Christian na Islamic). Likachukuliwa Neno la kwanza Chris katika Christian, likaunganishwa na Neno la katikati “slam” kutoka katika Islamic. Kuunda Chrislam

Ni imani iliyotokea, kwenye nchi ya Nigeria miaka ya 1970.  Kutokana na kutokuwa na maelewano ya kiimani baina ya jamii hizi mbili za dini, ikitambulika kuwa Taifa La Nigeria ndio lenye idadi ya watu wengi barani Africa, ni kama Nusu kwa Nusu, dini hizi mbili ndio zimechukua jamii kubwa ya watu.

Hivyo waanzilishi wa umoja huu walikuwa na malengo ya kuondoa tofauti zao za kidini, hususani zilizo toka katika mataifa ya magharibi na ya mashariki ya kati, na vile vile pia kwasababu hizi ndio dini kubwa duniani, basi pia zikiunganika wanaweza kusaidia kuushinda upagani kwa kubwa sana.Na ukweli ni kwamba imani hii imekuwa maarufu sana duniani, hususani kwa kipindi cha sasa.

Waanzilishi waliazimia kuufanya umoja huu, wakidhania kuwa, sehemu kubwa ya dini ya kikristo inatajwa katika Quran, wakimtaja Yesu mwenyewe pamoja na baadhi ya manabii wa kale, kama Ibrahimu na wengineo. Lakini pia uislamu na ukristo pia unamwingiliano mkubwa wa kitamaduni. Hivyo kwa mujibu wa hoja zao hakuna sababu ya kuwa hakuna tofauti yeyote katika mashindano ya kidini

Lakini je! Umoja huu, mbele za Bwana unakubalika?

Hivyo Imani ya Kikristo pamoja na Imani ya dini ya kiislamu haviwezi kuchanganyika, ni sawa na maji na mafuta. Kwasababu kiini cha imani ya ukristo ni KRISTO mwenyewe, na kwamba mtu hawezi kwenda mbinguni pasipo kumwamini YESU kama mwokozi PEKEE anayewaokoa wanadamu. Jambo ambalo haliendani na dini ya Kiislam, katika imani ya kufika mbinguni, ambapo kwao Kristo ni kama mmojawapo wa manabii tu wengine. Na hivyo mbingu si kupitia Kristo, bali kupitia matendo mazuri kama vile kukaa mbali na uovu na Mambo mengine.

Uislamu haumtambui Kristo kama Mungu, huamini kuwa yoyote anayemfanya Yesu ni Mungu, ni makufuru, kwasababu Mungu hajazaa, wala hajazaliwa. Hivyo aaminiye kwa Yesu ni Mungu, hawezi ingia peponi.

Kwa hoja hizii, uislamu na ukristo ni imani mbili tofauti kabisa, ijapokuwa zitaonekana kushabiana baadhi ya desturi, lakini bado hazitaweza kuletwa pamoja kuwa dini moja

Je! Hatupaswi kuwa waamini wa Chrislam?

kama Mkristo ulieokolewa kwa damu ya thamani na kuoshwa makosa yako na kupokea Roho Mtakatifu,, imani yako haipaswi kuchanganywa na Imani nyingine yoyote, ukifanya hivyo ni Kosa la kiimani. Sisi tunaamini, wokovu ni kwa kupitia Yesu Kristo anaotupa BURE kwa neema katika kumwamini Yeye, kwa kifo chake pale msalabani.

Tunamtegemea Kristo kutuokoa, kutupa nguvu ya kuishi maisha makamilifu, kutuongoza, kwa asilimia mia. Hivyo hatuna msingi au tegemeo lingine nje yake yeye. Na hata hivyo kibiblia, yeyote asiyekubaliana na Kristo Yesu, kama ndiye mwokozi pekee. Huyo ni mpinga-Kristo.

Hivyo kwa kumalizia ni kuwa wewe kama mtu ulio okolewa tayari, usijihusishe na imani nyingine yoyote nje ya Kristo Yesu mwokozi wako.

Matendo 4:12  Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo

Bwana awabariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx11

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *