elewa maana ya Yakobo 4:9 “Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza

Maswali ya Biblia No Comments

Biblia inasema katika Yakobo 4:9
Kwamba kucheka kwetu kugeuzwe kuwa maombolezo, je Mungu hapendi tuwe tunafurahi? Au maana yake ni nini mstari huu?

Maandiko yanasema…

Yakobo 4:9  “Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu”.

Kicheko kilicho tajwa hapo ambacho kinapaswa kigeuzwe kuwa maombolezo sio kicheko cha mambo mazuri, kwamba umeona watu wameokoka, wakaponywa magonjwa wame pokea roho mtakatifu na ukafurahi na kurukaruka Kwa shangwe kushangilia na kucheka, kwamba ndio kicheko hicho kibadilike kiwe maombolezo!

Sivyo kabisa Bali kicheko kinachozungumziwa hapo ambacho ni sharti kibadilike na kuwa maombolezo ni kicheko cha mambo maovu na mabaya (yaani dhambi). 

yaani Mtu anapocheka baada ya kupata mali za dhuluma, kicheko kama hicho ndicho biblia inachosema kuwa kinapaswa kibadilike kuwa kuomboleza, Kicheko mtu anachokipata baada ya kumlaghai na kumdanganya mwingine au ukazini na mke wa mwinzio, au kula rushwa au hata kuua mtu au kufanya jambo lingine lolote baya hicho kicheko kinapaswa kibadilike na kuwa huzuni.

Sawa basi mtu anapotambua makosa yake hapaswi tena kufurahia Yale mabaya anayoyatenda au aliyokuwa anayafanya, badala yake inabidi sasa aomboleze, mtu aliyekuwa anazifurahia uzinifu na kuhufurahia pale anapomjua Yesu, basi sasa asiendelee kufurahia maisha hayo bali aomboleze kwa kutubu na kujutia alichokuwa anakifanya.

Sasa ni kwanini ni Bora sana kuomboleza na kutubu kwa mabaya, badala ya kushangilia na kufurahia katika mabaya?

Ni kwasababu Bwana Yesu alisema ole wao wachekao sasa maana wataomboleza na kulia.

Luka 6:25 “… Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia”.

Sasa basi ni bora leo kuomboleza na kulia kwaajili ya dhambi na maovu ili Mungu atupatie rehema na siku za mwisho tuweze kuokolewa na mateso pamoja na moto wa milele, kuliko leo kucheka na kufurahia mambo mabaya lakini mwisho wa siku tunaenda kwenye liwe ziwa la moto.

Swali ni je! Mimi na wewe leo tunafurahia nini na kuombolezea nini?

Ila je ni hizo anasa ndizo unazozifurahia?, ni uchawi na uongo au masengenyo ndizo unavyofurahia?, je ni fedha za dhuluma ndizo zinazokupa kicheko?, je ni uzinzi ndio unaokuburudisha? Je ni kuanguka kwa wengine ndiko kunako kupa fuhara sana.

Kumbuka neno la Mungu litabaki kuwa lile lile siku zote kuwa “ole wa wanaocheka sasa maana watalia”

Tubu ukaoshwe dhambi zako leo kwa kumwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo.

Yakobo 4:7  “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

8  Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

9  Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.

10  Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza”.

Bwana atusaidie

Washirikishe na wengine ujumbe huu. Maana ni upendo.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *