Fahamu maana ya ukaufu kibiblia (kumbukumbu 28:22)

Maswali ya Biblia No Comments

Kumbukumbu 28:22

“Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa UKAUFU, na kwa KOGA; navyo vitakufukuza hata uangamie”

Swali: kutokana na Andiko hilo Je! Ukaufu ni Nini? Na koga ni Nini?

Ukaufu ni ugonjwa wa mazao unaotokana na fangasi,na kuleta utandu. Linapopata zao jamii ya nafaka husababisha mabaka mabaka, kukauka hatimae kutozaa kabisa.

Koga ni ugonjwa unasababisha utandu mweupe katika mimea, unapolipata zao la chakula, zao huathirika kufikia kufa kabisa.

Bwana anatuambia kuwa tunapomwacha yeye na kuigeukia au kuisujudia au kuabudu miungu mingine, Basi tunakuwa tumefungua milango ya laana katika maisha yetu. Maana tutapigwa sisi pamoja na mazao yetu ya Mashambani, tutapigwa kwa magonjwa, misiba, majanga ya nchi n.k

Mfano ni hayo magonjwa tajwa hapo juu kama vile kifua kikuu, kuwashwa, homa hayo ni kwetu lakini Ukaufu na koga hayo ni kwa Mazao ili tusipate hata chakula! Kwa ukengeufu huo.

Madhara mengine ni kama hali ya moto na Upanga; Yaani vipindi vya Ukame na jua Kali pamoja na Vita! Au Upanga! Ama umwagaji damu na kujitumainisha katika Maovu. tusome…

Kumbukumbu la torati 28:58

“Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, Bwana, MUNGU WAKO;

59 ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.

60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.

61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa”.

Endapo itakuwa ni kinyume chake yaani kwa KUMTII BWANA MUNGU WETU na kuenenda katika mapenzi yake, tutafanikiwa sana na kufungua milango ya Baraka za Mbinguni; na hatutapatwa na hayo majanga katika kumbukumbu ( 28:1-14).

Bwana na Atusaidie na kutuneemesha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *