Fahamu maana ya waibao watu, 1timotheo 1:10

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU, tusome… 

1 Timotheo 1:8-10

[8]Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;

[9]akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,

[10]na wazinifu, na wafiraji, na WAIBAO WATU, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

Dhambi ya wizi si katika vitu tu au mali ipo hata katika watu,hii ndiyo ipo juu zaidi ya wizi wa aina nyingine na si kwa wakati huu tu ni tangu zamani ambapo watu waliiibiwa kwa malengo tofauti tofauti lakini mojawapo ilikuwa ni kuwauza kwenda vitani na wakati mwingine kwa ajili ya kuwa watumwa. Jambo hili lilitokea katila bara la Africa mnamo karne ya 17,wakati huo waafrika waliibiwa na kupelekwa bara la ulaya.

Hivi sasa wizi wa namna hii umekuwa na Lengo lingine ambalo ni baya zaidi, watu wanaibiwa lakini si kwa ajili ya kupelekwa utumwani bali wanapelekwa kufanya kazi za ukahaba, wengine huiba watu na kuwaua na waibaji huchukua baadhi ya viungo vyao na kuvitumia katika mambo ya  ushirikina, viungo vingine kama figo huuzwa ili wajipatie fedha.

Tunaposoma maandiko, agano la kale tunaona dhambi hii ilkuwa na adhabu kubwa nayo ni kifo..

Kumbukumbu la Torati 24:7

[7]Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Lakini sasa hivi katika agano jipya haturuhusiwi kuwaua waibao watu badala yake tunatakiwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili kuilinda jamii na kudhibiti vitendo hivyo…

Jambo lingine la kufanya kuzuia uovu huu ni kumuomba Mungu aondoe roho hii mbaya miongoni mwa watu.

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *