Jina la Bwana wetu Yesu Kristo na libarikiwe.
Epafrodito alikuwa ni miongoni mwa watendakazi wa makanisa ya huko filipi, na alijulikana kama Mhudumu wa mahitaji ya Mtume Paulo.
tunaona ni upendo mkubwa kiasi gani kanisa la filipi linaonesha kwa mtume Paulo alipokuwa Rumi kifungoni. Lilimkumbuka kwa mahitaji Yake ya kifedha, Sasa ndipo anachaguliwa huyu epafrodito kusafiri umbali mrefu kiasi kile na kiasi kikubwa cha fedha mpaka huko Rumi. Hii ilikuwa ni kawaida yao kutimiza mahitaji ya Mtume Paulo mara kadhaa, kama tunavyoona katika wafilipi 4:16,18
Wafilipi 4:18 ” Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.”
Lakini mbeleni katika waraka wake Paulo anaelezea Hali ya ndugu huyu ambaye alimwita Mtume, kwa jinsi ilivyokuwa dhoofu nusu ya kufa pindi akiwa katika kazi hiyo ya kumhudumia Paulo, Lakini pamoja na hali hiyo bado hakuacha huduma yake.
Tunasoma pia katika hali yake hiyo ya Ugonjwa Mungu alimponya, Haijawekwa wazi aliugua ugonjwa Gani lakini tunaambiwa ulimfanya awe dhoofu sana kiasi cha kudhaniwa kuwa ni ‘WA kufa tu’.
Baada ya kumaliza huduma yake ndipo tunaona Mtume Paulo anaandika waraka wake kwa wafilipi na kuufikisha kwao kwa kumtumia Mtumishi huyu Epafrodito,
Wafilipi 2:25 “Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu.
26 Kwa kuwa alikuwa na shauku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi.
27 Kwa maana alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni.
28 Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma, ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu.
29 Mpokeeni, basi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.
30 Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akaponza roho yake; ili kusudi ayatimize yaliyopungua katika huduma yenu kwangu.”
Tunajifunza Nini kwa Mtumishi wa Mungu Epafrodito?
Upendo wa kujali Hali za Wengine
Biblia imeandika upendo hautafuti mambo yake wenyewe (1 Korintho 13). Epafrodito alikuwa tayari kufa na Hali yake Lakini askari mwenzie asipungukiwe mahitaji Yake, Mungu wetu anathamini sana Utume kama huu.
Tunajifunza pia habari za Huruma ya Mungu kuwa pamoja na hali yake kuwa nusu kufa, Mungu alimponya akawa Mzima.
Hata sisi Leo tunaweza fikia hatua madaktari wakahitimisha huyu kupona haitowezekana? Na kama ni ndio basi tumkumbuke Epafrodito, Labda Hali yako imekuwa ngumu na kusema hapa siwezi kuvuka; Mkumbuke Epafrodito. Hakuna linaloshindikana kwake Mungu wetu.
Ukiwa katika Utumishi wako usihofu matatizo ya kiafya, kifedha usitetereke, mwamini Mungu Usiache kumtumainia nae Atafanya.
Maran atha
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.