Maana ya zaburi 48:15 yeye ndiye atakaye tuongoza ni nini?

Maswali ya Biblia 1 Comment

Shalom. Karibu tuyatafakari Maneno ya Uzima

Zaburi 48:14

[14]”Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.”

Tunaona mwandishi akijivunia sifa ya Mungu wao wa milele.

Kwamba ndiye atakayewaongoza katika Mambo yote kwa njia sahihi na ya uzima, njia sahihi ya kupanda, kupigana vita na kujenga lakini kubwa zaidi ni kwamba hatowaacha Milele.

Tunaona ilikuwa hivyo kwa wana wa Israeli Jangwani Mungu alikuwa nao akiwaongoza nyakati zote kama nguzo ya moto na kama mawingu, akiwapelekea Malaika wake kuwalinda, aliwafundisha namna ya kupata faida katika kazi zao.

Aliwainulia waamuzi, Wafalme, Manabii na mwisho akawaletea masihi Mkombozi ambaye ni Ukamilifu wa yote. Anafanya Wema wote huu ikiwa ni kuonesha kiu ya kuwaongoza watu wake.

Sifa yake ni ile Ile na hata sisi Leo tunao ujasiri wa kusema ‘Yeye ndiye atakayetuongoza’ si kwa kitambo tu Bali mpaka mwisho wetu.

Alipokuja mkombozi hakutuacha mayatima Bali alituachia msaidizi naye huyo ndiye atakayetutia kwenye kweli yote naye ni Roho Mtakatifu.

Yohana 16:13

[13]”Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.”

JE umempokea Yesu maishani mwako? Kama bado wakati ni Sasa.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

One Reply to “Maana ya zaburi 48:15 yeye ndiye atakaye tuongoza ni nini?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *