TAMBUA UNAYEMTUMIKIA NI NANI NA ANATAKA NINI?.

Biblia kwa kina No Comments

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.

Somo hili ni muhimu kwako wewe mshirika unayeudhuria  kanisani kila jumapili na wewe pia muhudumu wa Madhabahuni ikiwa ni Shemasi,Mchungaji,Nabii muimbaji wa kwaya nk.

Watu wengi leo hii wanakwenda kanisani na wanatumika madhabahuni wengine lakini hawatambui ni nani wanayemtumikia na anataka nini?. Lakini kila mtu ukimuuliza unamtumikia nani ama anakwenda kwa nani atakwambia anakwenda kanisani kwa Mungu ama anamtumikia Mungu.

Kuna watu wako kanisani lakini wanamtumikia Mchungaji ama kiongozi Fulani ama mtu Fulani katika kanisa na sio Yesu Kristo lakini watu hawalitambui hili. na hili ni jambo muhimu (Siri kubwa sana iko hapa) sana unatakiwa kulitambua/kuijua kama mwamini.

Leo hii kuna watu wakikosewa/kukwazwa na Mchungaji(yaani mchungaji akateleza tu wala hakukusudia wakati mwingine kakukwaza hata pasipo yeye kufahamu maana yeye pia ni mwanadamu hajakamilika asilimia zote.) wanakasirika na wanaacha kwenda kanisani kabisa ama wanahama kanisa.

Kwa sababu tu mchungaji alimkwaza mahali Fulani ndio hataki kabisa kwenda kanisani. Lakini mwingine ameambiwa tu asogee kiti cha mbele yake anakwazika na anasema mwenyewe ndani yake

yeye ni nani anajifanya tena kuja hapa mwisho leo hawataniona tena nk

pasipo kutambua ama kujua kuwa Yule anamuelekeza vile ni Kristo maana yuko ndani yake.

Umewahi kujiuliza ni kwa nini mtu anachukua hatua za namna hiyo hata kuacha kwenda tena kanisani? Ni kwa sababu hajui anayemtumikia ni nani!, na kwa kawaida aliyekuwa akimtumikia hapo ni mchungaji ama shemasi nk. na baada ya kumkwaza basi anaona kwa akili yake kuwa ili amkomeshe asiende tena kanisani. Au asiiembi tena kwaya lakini je?

Anayemkomoa hapo ni mchungaji ama Mungu na ni nani  anaepata hasara? Natamani unaposoma ujumbe huu utafakari, umeshahama makanisa mangapi? Na sababu ya kuhama ni nini?,

Lazima ulitambue hili shetani anatumia mbinu nyingi sana ili tu kukuharibu akupate na pasipo kuwa imara katika imani atakupata tu.

Utakuta wakati mwigine mchungaji amekosewa na mtumishi mwenzake ama mshirika wake anaandaa somo la kuhubiri jumapili ama jumatano linamlenga mtu mmoja tu na kumsema kwa mafumbo.
wala Roho Mtakatifu hayuko kabisa hapo maana umefata akili zako na hujamfata Roho Mtakatifu. Unamaliza kuhubiri hapo wala hakuna mtu anayejengwa na kubalikiwa na somo.

Unapoacha kwenda kanisani kwa ajili ya mtu Fulani kakukwaza jua fika ulikuwa unaenda kanisani kwa ajili yake na sio kwa ajili ya Mungu. maana kama ungekuwa unaenda kanisani kwa ajili ya Mungu wala usingeshindwa kwenda ungeendelea kwenda hata usingejali zaidi ungezidi kumuombea na kutafuta suruhu maana unakuwa unajua unakwenda kanisani kwa ajili ya Mungu na sio kwa ajili ya mtu Fulani unakuwa unafahamu fika ni nani unaemtumikia?”

Ni muhimu sana kujua kinachokupeleka ibadani ni nini? Usifurahie tu kwenda ibadani na hujui kwa nini?

BAADHI YA MAMBO WATU YANAYOWAPELEKA KANISANI PASIPO WAO KUJUA.

Yako mengi sana lakini kama umesoma vizuri toka mwanzo wa Somo utakuwa umenielewa vizuri.

FEDHA.
Wakati mwingine mtu inayompeleka kanisani ni fedha. Akiyumba kiuchumi mambo yakaenda ambavyo hakutarajia anakata mahusiano yake na Mungu. Hapo mtu alikuwa anakwenda kanisani kwa sababu mambo yalikuwa ni mazuri yakiharibika anatafuta njia nyingine.

Ndugu yangu tambua kabisa na ni muhimu tuko hapa duniani ni lazima tu tutakutana na changamoto nyingi tu jua kabisa shetani anatuwinda kama dhahabu ya Ofiri. Usiku na mchana haachi kukuwinda je? Utaendelea kuhama hata lini.

MAVAZI.
Leo hii watu wengi sana hasa wanawake na mabinti wananuna na kukasirika sana wanapoambiwa wavae mavazi mazuri ya kujistiri. Wengine wanahama na makanisa kabisa kwa sababu wameambiwa hivyo, hawajui ni kwa faida yao na Yule wanayesema wanamtumikia anataka wajistiri lakini wao hawataki.

Ni Muhimu sana kumuelewa na kumfahamu unaemtumikia.

Tumtazame mtu mmoja ambaye yeye alimtumikia Mungu kweli na alitambua ni nani anaemtumikia.

DAUDI.
Daudi alitambua anayemtumikia ni nani? Ijapokuwa alikuwa akifanya kazi chini ya Mfalme Sauli lakini alijua ni nani napaswa nimtumikie. Ijapokuwa Daudi aliudhiwa mara nyingi na Sauli akakoswa koswa kuuwa karibu mara mbili kwa mkuki nk lakini angalia Daudi alitambua ni nani anayemtumikia na anataka nini ambaye ndie Yesu Mwenyewe.

Aliendelea kuwa ni myeyekevu chini ya Sauli wala hakutaka kumlipizia kisasi wala kumuuwa ingali alikuwa na nafasi hiyo ya kufanya hivyo lakini hakufanya hivyo. Na hata aliposikia Sauli amepatwa na mabaya hakuwa anashangilia bali alikuwa anaomboleza na kumsikitikia.

1 Samweli 18:11 “Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili.”

Mambo mengi sana Daudi alifanyiwa na Sauli lakini alikua ni mpole na mnyenyekevu. Na hakutaka kumlipizia kisasi hata alipopata nafasi ya kufanya hivyo.

Na hii haikumzuia Daudi kumtumikia Bwana na kuwaokowa Israeli ni kwa sabau alijua anayemtumikia ni nani na anataka nini.

Je! Ni nani unayemtumikia? Tafakari kwa kina kisha ukiona kuna mahali hapako sawa tengeneza njia zako. Hizi zote ni tabia za uchanga kiroho mpe Yesu nafasi ukue na kukomaa zaidi kiroho ili umtambue zaidi na ujijue kwa nini uko hapo ikiwa ni wewe Mshirika au wewe unayehudumu madhabahuni.

MARANATHA.

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *