Shalom.
1 Wakorintho 6:2-3
2 “Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?”
Kwa sababu Yesu Kristo alitwaa jinsi ya mwili na si ya malaika Wala kiumbe chochote kingine, Watakatifu wamefananishwa na Yesu Kristo. Kama Maandiko yanavyomtaja kama mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi ambao ndio sisi
Waebrania 2:16 ” Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake”.
Kama tunavyosoma ya kuwa Mungu alimpa vitu vyote vya Mbinguni na duniani, na kuzimu; Alimpa pia na hukumu yote (Yohana 5:22), tusome pia
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
Hivyo kwakuwa anayo hukumu ya vyote yaani vichafu na visafi, vilivyopo na vijavyo, ni wazi kuwa pia malaika wote watakatifu na walioasi wote watahukumiwa na yeye kutokana na njia zao.
Kama watakatifu watakavyoketi pamoja Na kristo katika hukumu (Ufunuo 3:21) maana watasimama kama ndugu zake. Ndio maana Paulo anasema hamjui ya kuwa Mtawahukumu malaika.
Hivyo ni kweli watakatifu watahukumu malaika; watakatifu watatukuzwa zaidi Lakini walioasi hatma ni katika ziwa la moto
Ufunuo 20;4
” KISHA NIKAONA VITI VYA ENZI, WAKAKETI JUU YAKE, NAO WAKAPEWA HUKUMU; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.”
Hivyo basi, watakaoshinda na kuketi pamoja naye katika kiti Cha enzi hao ndio watakaounukumu Ulimwengu na malaika.
Kumbuka mamlaka hayo watapata wale tu watakaoshinda, na mamlaka haya tutayapata baada ya maisha haya, kama ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo (Waebrania 2:9)
Nasi tujitahidi tuushinde!
Tusome Maandiko haya..
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Ubarikiwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.