Ufahamu utaratibu wa kutoa fungu la kumi.

Maswali ya Biblia No Comments

 

Kuna maswali ambayo yamekuwa  yanaulizwa kuhusu zaka, haya ni maswali 8 ambayo yanaulizwa sana

1.Nani anayetakiwa kutoa fungu la kumi?

2.Fungu la kumi linatolewa katika mtaji au faida?

3.Zawadi tunazopokea tunapaswa kuzitolea fungu la kumi?

4.Fedha ya mkopo inatakuwa kutolewa fungu la kumi?

5.Ikiwa mshahara wangu ni milioni moja lakini kuna makato ya serikali mfano kodi na pspf, na pesa nayopokea mkononi ni laki 7 je fungu la kumi natoa katika laki saba au ile milioni moja?

6.Je nikipokea mshahara ambao haupo katika mfumo wa fedha mfano ng’ombe, kuku, fungu la kumi nitalitoaje?

7.Fungu la kumi naweza kuliweka kuwa deni? Yaani badala ya kutoa kila siku nikakusanya kwa pamoja na kutoa mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka?

8.Kimaandiko fungu la kumi linatakiwa kupelekwa wapi? Kuna ulazima wowote wa kutoa fungu la kumi?

Tuanze kuyajibu maswali yetu ili tupate uelewa mzuri kuhusu fungu la kumi(zaka)

1.Nani anayetakiwa kutoa fungu la kumi?

Fungu la kumi linatolewa na mtu yeyote aliyeokoka bila kujali umri wake jinsia wala hali yake ya kiuchumi. Ikiwa unafanya kazi au hufanyi, kutoa fungu la kumi ni lazima.

2.Fungu la kumi linatolewa katika mtaji au faida?

Tunatoa fungu la kumi katika faida sio mtaji. Mfano una mtaji wa laki moja ambayo kila siku unapoifanyia kazi unapata faida ya elfu 10 basi zaka utaitoa katika hiyo elfu 10 ambayo itakuwa ni kiasi cha shilingi elfu moja.

3.Zawadi tunazopokea tunapaswa kuzitolea fungu la kumi?

Ikiwa utapokea zawadi na kuifanya kama mtaji basi hautatoa zaka lakini utatakiwa kutoa zaka kutoka katika faida utakayoipata. Endapo utaamua kuiweka zawadi hiyo katika matumizi ya kawaida ya kila siku basi unapaswa kuitolea zaka kabla ya kuitumia.

4.Fedha ya mkopo inatakuwa kutolewa fungu la kumi?

Ikiwa umechukua mkopo ili uufanye kama mtaji wa biashara hapo hutatoa zaka utasubiri ufanye hiyo biashara na faida yake ndiyo utakayoitolea zaka. Na ikiwa umechukua mkopo kwa lengo la kutumia katika matumizi ya kujikimu kama vile chakula, mavazi, malazi n.k basi mkopo huo tunaufananisha na mshahara hivyo unapaswa kutoa zaka kutoka katika huo mkopo.

5.Ikiwa mshahara wangu ni milioni moja lakini kuna makato ya serikali mfano kodi na pspf, na pesa nayopokea mkononi ni laki saba fungu la kumi natoa katika laki saba au ile milioni moja?

Hapa zaka utatoa katika milioni moja sio katika laki saba, ina maana kwanza zaka hapo itakuwa ni laki moja.

6.Je nikipokea mshahara ambao haupo katika mfumo wa fedha mfano, ng’ombe, kuku, fungu la kumi nalitoaje?

Ukimpokea ng’ombe na kumfanya kuwa mtaji wa biashara zaka utaitoa ukipata faida kutokana na shughuli ambazo utazifanya kupitia ng’ombe huyo. Mfano ukiuza maziwa basi faida itakayopatikana hiyo ndiyo utakayotoa fungu la kumi.

Ikiwa ng’ombe huyo utamfanya kuwa kitoweo, basi tafuta thamani yake kisha uitolee fungu la kumi,mfano akiwa na thamani ya milioni moja basi utatoa laki moja kuwa fungu la kumi. Endapo utakosa thamani yake basi utachukua sehemu ya kumi katika nyama zake.

7.Fungu la kumi naweza kuliweka kuwa deni? Yaani badala ya kutoa kila siku nikakusanya kwa pamoja na kutoa mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka?

Ndio unaweza kufanya hivyo ikiwa kuna sababu za msingi. Yawezeka unapata faida ndogo na zaka yake inakuwa kiwango cha chini mfano shilingi 50 au 40 au 20 kiuhalisia huwezi kutoa zaka hiyo kila siku kwa sababu hata hizo sarafu kwa sasa hazitumiki, hapo ndipo utazikusanya kwa wiki au kwa mwezi na kuzitoa kwa pamoja.

Hata hivyo maandiko hayajaweka ratiba maalumu ya utoaji wa zaka, basi ikiwa mtu ataamua kutoa kwa wiki au mwezi atakuwa hajakosea kitu cha msingi ni kutoa kiasi chote kwa uaminifu. Lakini itakuwa vizuri zaidi ikitolewa mapema ili kuondokana na mlundikano wa madeni.

8.Kimaandiko fungu la kumi linatakiwa kupelekwa wapi? Kuna ulazima wowote wa kutoa fungu la kumi?

Kwa jibu la swali la 8 fungua hapa,

NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?

Ubarikiwe na Bwana

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *