Shalom.
Swali hili halikuanza kuwatatiza watu Leo, hata Zamani hizo kipindi Cha Yesu Kristo duniani liliulizwa pia. Tusome..
Luka 13:23 ″Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika MLANGO ULIO MWEMBAMBA, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. ”
Imeandikwa na katika injili ya mathayo..
13 “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”
Kulingana na Maandiko, Wanaookolewa ni Wachache, maana njia iendayo uzimani imesongwa sana na mambo ya Ulimwengu huu kama tamaa ya fedha, uasherati na Uzinzi, wimbi kubwa la Manabii wa Uongo wanaoipotosha njia hiyo na kufanya watu wapotee zaidi, Watu Leo wanapima utakatifu kwa mafanikio ya kimwili kuliko kupima Matendo ya mtu hivyo kupelekeka watu kugeukia Mali na kuacha kutumia Neno la Mungu.
Yesu pia alitolea mfano wa siku za Nuhu kwamba ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mara ya pili. Kipindi Cha nuhu waliokoka 8 pekee katika wote waliokuwapo duniani wakati huo, mfano mwingine ni kipindi Cha Luthu! Sasa Je waliokoka wangapi kipindi Cha Luthu? Ni watatu pekee kati ya wote waliokuwapo kipindi hicho! Kizazi chetu Yesu emekifananisha na kizazi Cha Nuhu.
Sikiliza wapendwa, tujitahidi kwa nguvu zote kupita mlango ule ulio mwembamba, Maana ni dhahiri watakaookolewa kipindi hiki Cha mwisho ni WACHACHE!
Tugeukie mafundisho ya awali ya mitume, ule Ukristo wa kale.
Mwanamke wa kikristo vaa na enenda kwa kumtukuza Mungu, kuvaa suruali, vimini, make-up na ma lipstick ni misimamo ya kidunia, Mwanaume wa kikristo acha matukano, Ulevi, kuvuta sigara Wala kupenda Yale yanayopendwa na Ulimwengu huu.
Je? Itakufaidia Nini kupata vitu vyote Ulimwengu mzima na kupata hasara ya Nafsi yako? Hakuna mbadala katika Hilo!
Kuwa macho Anza kutafuta Leo maarifa ya Neno la Mungu ili usijiliwe Kama mwivi katika siku Ile.
Amen
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii. Au unaweza fungua somo hili kwa mwongozo wa sala ya toba>> https://rejeabiblia.com/kuongozwa-sala-ya-toba/
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.