Malimbuko ni aina gani ya sadaka?

Maswali ya Biblia No Comments

 

Malimbuko ni sadaka inayotolewa kwenye kitu cha kwanza kupatikana, au kuzaliwa, au zao la kwanza Katika vitu vyenye uhai kama watoto, wanyama,ndege n.k na vitu visivyo na uhai kama mazao, fedha, n.k, kwa lugha nyingine inajulikana kama “first fruits”…enzi za agano la kale mtoto wa kwanza wa kiume kuzaliwa alitolewa malimbuko kwa Bwana.

Tazama Mwanzo 49:3…

Mwanzo 49:3 “Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu”.

Mungu aliagiza wana wa Israeli watoe sadaka hiyo kati ya uzao wao, na wanyama wao, na mazao yao wafanye vivyo hivyo..mfano kama ni mnyama amezaa kwa mara ya kwanza, basi hicho kilichozaliwa ni cha Bwana, au kama ni mazao ya kwanza kupatikana shambani moja kwa moja yalipelekwa yote mbele za Bwana,
Soma tena katika….

Mambo ya Walawi 23:9 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu;”

Wana wa Israeli walipewa hayo maagizo ya kutoa sadaka ya namna hiyo(malimbuko) katika uzao wa wana wao, wanyama wao, mazao yao lengo ni ili wamkumbuke Mungu katika yote ambayo Bwana anawabarikia aiza ni mashambani, au katika mifugo walipaswa warudishe kwanza shukrani kwa Bwana ndipo waendelee kutumia zao la pili..

Kwahiyo zao la kwanza daima lilikuwa la Mungu kwani Mungu ni wa kwanza katika yote na pia ndiye anayetoa huo uzao na hayo mazao mashambani kwa kunyeshea mvua, Kwahiyo anastahili kupewa kile cha kwanza kabisa kilichokuja au kilichozaliwa na hayo mengine yatakayofuata ni ya kwao.

JE KULIKUWA NA BARAKA ZOZOTE KATIKA KUTOA HIYO SADAKA YA MALIMBUKO?

Jibu ni ndio! Baraka zilikuwepo tele, kwasababu siku zote kitu cha Kwanza kumtolea Mungu kina nguvu kuliko cha Pili. Kwa mfano ukiangalia tu katika maisha ya kawaida, nguo mpya ambayo haijavaliwa na mtu ina thamani zaidi, na ubora zaidi kuliko ile ya Mtumba.

Hata kiongozi wa kwanza wa nchi, huwa anapewa heshima kubwa Zaidi kuliko viongozi wengine wanaofuata. Vivyo hivyo na sadaka ya kwanza kabisa inayoletwa mbele za Mungu ina nguvu kubwa zaidi kuliko zinazofuata..Na sadaka hiyo ya kwanza ndiyo hiyo inaitwa “malimbuko”.

Vilevile sadaka ya malimbuko ndiyo inayobariki kazi yote inayofuata, mshahara wa malimbuko ndio unaobariki mishahara mingine yote inayofuata. hapo chini kidogo tutakuja kuona ni kwa namna gani Kristo aliitwa limbuko lao waliolala, ikasababisha baraka kwa wote watakaolala kama yeye.

JE KATIKA AGANO JIPYA WAKRISTO TUNAPASWA KUTOA SADAKA YA MALIMBUKO?

Ndio tunapaswa kutoa!. Kama vile tunavyotoa fungu la kumi, vivyo hivyo na malimbuko nayo ni lazima..Na baraka zake ni zile zile…Kama tulivyoona kuwa kitu cha kwanza ni bora kuliko kile cha pili, hata kama hicho cha pili kitakuwa na kingi kiasi gani..lakini hakiwezi kuzidi kile cha kwanza.

Na Roho Mtakatifu anatushuhudia ndani yetu kabisa.. kuwa kama sio Mungu kubariki hiyo kazi ya mikono yetu tusingeambulia chochote, kwahiyo ni lazima tumheshimu Mungu na kumwonyesha kuwa yeye kwetu ni wa KWANZA kwa vitendo! hivyo hatuna budi kumpa Malimbuko yetu.

JINSI YA KUTOA MALIMBUKO;

Kama umeajiriwa au umejiajiri, Mshahara wa Kwanza unaoupata unapaswa upeleke kwa Bwana. Usiogope kupungukiwa, wala usiwaze waze utapata vipi fedha, yeye aliyekupa hiyo kazi anajua zaidi kuliko wewe, anasema maua haifanyi kazi na bado hayasokoti yanazidi kupendeza tu.

Kitu ambacho hata Sulemani katika fahari yake, hajawahi kuvikwa vizuri kama mojawapo ya hayo!. Kama Mungu anayavisha maua ya kondeni vizuri hivyo je si zaidi sisi?. (Mathayo 6:28)…hivyo usiangalie mazingira yanayokuzunguka mtolee Bwana sehemu ya kwanza.

Na vilevile faida ya kwanza ya Biashara yoyote iliyo halali uliyojiajiri ni hivyo hivyo, sehemu ya kwanza ya mazao yako ya shambani, kama umevuna gunia 10 mpelekee Bwana zote, mifugo yako imezaa wazaliwa wa kwanza mpelekee Bwana, au ibadilishe katika fedha, uipeleke nyumbani kwa Bwana.

Kumbuka kama umeshatoa mzaliwa wa kwanza wa mfugo wako, hao wengine hupaswi kutoa kama malimbuko. Hao utatoa tu kama sadaka na kwa jinsi Bwana atakavyokujalia. Na kwa jinsi utakavyopenda wewe kutoa, haina masharti!

Kumbuka pia kama umeacha kazi fulani na kwenda kuanza nyingine, ambayo inazalisha kwa namna nyingine, na ina mkataba mwingine wa kukuingizia kipato, hapo ni lazima utoe tena limbuko kwa hiyo kazi mpya ulioanza. Kwa ulinzi wa kazi yako.

NI KWA NAMNA GANI YESU KRISTO NI LIMBUKO LAO WALIOLALA.

Tunajua Bwana wetu YESU ndiye wa kwanza kufa na kufufuka na baada ya hapo akaishi milele..kama tu ilivyo kwa watakatifu wote waliolala na wanaolala sasa..ipo siku watafufuliwa na kwenda kuishi na Bwana Yesu milele kama maandiko yanavyosema(1Wathesalonike 4:16-17),

Kwa maana hiyo mtu wa Kwanza kufufuliwa alikuwa ni Kristo! labda utauliza mbona Lazaro alifufuliwa? Ndiyo Lazaro alifufuliwa na Yesu mwenyewe lakini alikufa tena…Hivyo ufufuo wake haukuwa na nguvu ya umilele, ipo siku atafufuliwa tena na watakatifu wengine na kuishi milele kama Kristo anavyoishi sasa,.. Kwahiyo Yesu Kristo ni mzaliwa wa kwanza wa waliokufa(LIMBUKO)

Kama vile Mungu alivyomfufua mwanaye Kutoka katika wafu ili awe limbuko kwa wote walio katika wafu, na sisi pia tuliomwamini tutakaokufa kama yeye, tunapata hiyo neema ya ajabu ya kufufuliwa katika siku ile ya ufufuo.

Maana yake kama si Mungu kumtoa mwanaye wa pekee Yesu Kristo afe kwa ajili yetu na baada ya kufa akampandisha tena juu kaburini na akapaa mbinguni anaishi sasa milele, Haleluya!. Kama si Mungu kumtoa awe sadaka ya kwanza(limbuko) sisi wengine tusingepata hiyo baraka ya kufufuliwa, ila sasa kupitia Kristo tunayo hiyo ahadi kuu ya kufufuliwa na kuishi milele.

1Wakorintho 15:20 “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.

21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.

22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.

23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.”

Soma pia…

Wakolosai 1:18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.”

Si umeona faida ya kutoa sadaka ya”malimbuko” inasababisha mazao mengine yaliyosalia kubarikiwa..kama vile Kristo alivyotolewa kuwa limbuko lao waliolala, na sisi pia tuliomwamini tukifa kama yeye, na sisi tunapokea baraka ya kufufuliwa kama Mungu alivyomfufua, na zaidi tunakuwa na baraka tele ikiwemo uzima wa milele,

Kwahiyo tunalo tumaini la ufufuo, kwasababu yeye amefanyika kuwa mtangulizi wetu, na vivyo hivyo hata kwenye shughuli zako, kazi zako, biashara yako, kilimo, n.k, unakuwa na tumaini la kufufuliwa upya iwapo imeelekea kufa, ila hilo litafanyika tu endapo umetoa limbuko ile siku ya kwanza ulipoanza kupata faida kwenye hiyo kazi uliyoipata, je mshahara wako wa kwanza ulipeleka mbele za Mungu!. au kwenye mazao uliyovuna mashambani

Je siku ya kwanza ulipovuna kile ulichopata ulikuwa mwaminifu kupeleka mbele za Bwana kutoa kama sadaka ya malimbuko!. au pengine ni biashara.. ile faida ya kwanza uliyoipata kwenye hiyo biashara je ulipeleka mbele za Bwana kama sadaka ya malimbuko!.. chochote kile ambacho kinakupatia kipato, je! Ulitolea malimbuko kama sadaka ya utangulizi siku ile ulipoianza hiyo kazi,

Ila pia pamoja na hayo yote! Ni lazima ujue iwapo utakuwa unazingatia kutoa sadaka ya malimbuko kwa uaminifu na sadaka nyinginezo…ni vyema ufahamu kuwa kama upo nje ya wokovu (Kwa maana kwamba kama hujamaanisha kutubu dhambi zako na kumpokea Bwana Yesu) sadaka zako haitakufaidia kitu..isipokuwa unafanya machukizo kwa Mungu, unapaswa uwe ndani ya wokovu kwanza ndio mengine yafuate,

Unapaswa udhamirie kabisa ndani ya moyo wako kujikana na kuamua kumfuata Bwana Yesu.. unapaswa kuangamiza nafsi yako kwa habari ya anasa na starehe za ulimwengu kama Bwana Yesu alivyosema katika “Marko 8:35”, kabla hujaingia kumtolea Mungu kubali kwanza kuacha udunia, kubali kunyima nafsi yako vile ambavyo unaifurahisha na kushibisha, kama ni ulevi, uasherati, kutazama picha za ngono(pornography), kujichua (mastabartion) usagaji, uongo, usengenyaji,rushwa, kamari, n.k, kubali kuangamiza nafsi yako kwa habari ya kuacha hayo yote,..

Kama wewe ni mwanamke dhamiria ndani ya moyo wako kuchoma hizo vipodozi, lipstick, hayo mawigi, hizo vimini, hayo masuruali kwa kuwa ni machukizo kwa Mungu (Kumbukumbu 22:5), hayo mavazi ya kikahaba tupa zote, baki katika uasili wako (natural), kabla hujaenda kumtolea Mungu hizo sadaka.. hakikisha kwanza wewe mwenyewe umetoa mwili wako kuwa dhabihu takatifu (Warumi 12) ndipo utoe sadaka zinginezo kama hiyo ya malimbuko,..

Fahamu kuwa Mungu wetu sio mkusanyaji wa mapato, Kwamba ni lazima tu achukue kodi ya mapato zako, pasipo kujalisha usafi wako wa mwili na roho (kwamba uwe mwovu au usiwe mwovu ni lazima ulipe kodi!.)

Mungu wetu hafanyi kama wafanyavyo TRA kwasababu tayari anayo kila kitu, hivyo tunavyotoa ni kwa ajili yetu, sisi ndio tunahitaji kubarikiwa, na hapendezwi na sadaka ya mtu mwovu..kama mtu anafanya kazi ya ukahaba, au ya anauza bar, na bado anamtolea Mungu katika kazi hiyo ..ni heri asifanye hivyo, kwani kufanya hivyo ni machukizo mbele za Mungu, hiyo sadaka inamchukiza Mungu.

Neno la Mungu linasema…

Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili.”

Hivyo kama hujatoa maisha yako kwa Kristo umechelewa sana na mlango wa neema hivi punde itafungwa!. ni vyema ufanye maamuzi sahihi ya kumpokea Bwana Yesu ingali bado neema ipo,..unachopaswa kufanya ni kudhamiria kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi na tamaa zote za ulimwengu, unaamua kabisa kugeuka na kuacha Kwa vitendo yale yanayomchukiza Mungu,

Fanya maamuzi ya kuacha vyote, Neno la Mungu linasema katika..

(Matendo 19:19 “Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote;…)

Na wewe kusanya hirizi zako, chupa za pombe, mavazi ya kikahaba kama hizo vimini, nguo za kuchora mwili, na hayo mapambo ya kidunia (vipodozi, lipstick, mawigi, mahereni,n.k) na kila namna ya machukizo.. kusanya vyote uvichome kabisa na wala usivirudie tena, tubu kwa kumaanisha ili Bwana Yesu aingie ndani yako,

Hizo picha za ngono na miziki ya kidunia ambayo umejaza kwenye simu yako futa zote usibakize hata moja, kata mawasiliano na watu unaofanya nao uasherati na usengenyaji futa namba zao ikibidi, rudisha vitu ulivyoviiba, au ukivyochukua kwa hila rudisha na omba msamaha, patana na ndugu yako uliyekosananaye, tengeneza na Bwana Yesu ndugu yangu kabla hujachelewa..

Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na Bwana Yesu amekaribia kurudi, na hata usiposadiki kuwa hizi ni siku za mwisho, fahamu pia hujui siku za kuondoka kwako hapa duniani na biblia inasema baada ya kufa ni hukumu (Waebrania 9:27) Sasa ukiondoka katika hali yako hiyo ya dhambi, iyo hali ya kupenda dunia,..je huko unakokwenda utaenda kuwa mgeni wa nani? na Mungu anasema hafurahii kufa kwake mtu mwovu ni afadhali aghairi akaishi(Ezekieli18:23) maana yake ni dhahiri mtu akifa kwenye dhambi ni moja kwa moja ataenda kuzimu

Huko ambapo Bwana Yesu alisema na kiungo chako yaani mguu,mkono, jicho n.k, ikikukosesha ni afadhali uondoe kuliko kuwa na viungo vyote na ukaenda zako kutupwa jehanum ambapo kuna moto usiozimika na fuza ambao hawafi, soma “Marko9:43-48″ Pia soma habari ya tajiri na Lazaro katika Luka 16:19-33” biblia inasema kuzimu haishibi (Mithali 27:20) kila wakati inapokea maelfu,.. sasa njia pekee ya kuepuka huko ni kumpokea Bwana Yesu, yeye mwenyewe anasema “….

Mimi ndimi njia, na Kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” (Yohana14:6), utaingiaje kwenye hiyo njia (YESU), ni Kwa kudhamiria kutubu na kuacha vyote vinavyotusuia, vyote vya kidunia, anasa, starehe,na kawaida zote za kidunia unaamua kuacha, Kisha unaenda kubatizwa kwa ubatizo sahihi wa maji mengi na Kwa JINA LA BWANA YESU sawa sawa na Yohana 3:23 & Matendo 2:38, na baada ya hapo Roho Mtakatifu ataingia ndani yako na kukupa nguvu ya kuishinda dhambi na kukufanya uishi maisha matakatifu yanayompendeza Mungu,

Baada ya kuchukua hayo maamuzi na kufanya hivyo..basi hapo umeokoka na umekuwa mwana wa Mungu. unachopaswa kufanya ni kutafuta Kanisa la kiroho linalofundisha na kuhubiri maneno ya kweli ya Mungu yasiyoghoshiwa (vitabu 66) na utakatifu!. amani ya Bwana ikuongoze kujiunga hapo na kumwabudu yeye, pia atakuongoza kwa mengine yaliyosalia.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *