Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima ya mwokozi wetu Yesu Kristo.
Mtume Paulo alimaanisha nini kusema …”wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.”
Sasa kabla ya kuona Paul alikuwa akimaanisha nini katika mstari huo na wakina na nani alikuwa akiwalenga watu wa namna gani?
Ukianza kusoma vizuri kwa makini katika sura hii ya tatu Paulo anaelezea kizazi au kundi la watu litakalozuka katika siku hizi za Mwisho hawataji kwa majina lakini anaelezea sifa za watu hao au tabia zitakazokuwa zikionekana ndani yao..
2 Timotheo 3
1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
Ukiendelea kusoma katika mistari inayofata mpaka ule wa tisa utaona bado anaendelea kutoa tabia za watu hao watakuwa ni wa namna gani?.
Sasa ukianzia mstari wa saba(7) hapo kuna sifa nyingine ambayo ni muhimu sana kuifahamu na ndio ambayo tutakayokwenda kuiangalia kwa udani zaidi.
Sasa hebu tuisome tuone ni ya namna gani..
2 Timotheo 3:5-9
[5]wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
[6]Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
[7]wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.[8]Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
[9]Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
Maandiko yanasema…”wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.“
Watakuwa ni watu wenye bidii sana kujifunza na kukusanyika na kusoma sana na kuongeza maarifa mengi sana lakini hawataweza kuufikia ujuzi wa kweli.
Ujuzi ni nini?? Ni Hali ya kikifahamu kitu na kukielewa na kukifanya kwa umahaili na kwa ustadi mkubwa. Mtu mwenye ujuzi wa jambo fulani anaweza kukifanya kitu katika ubora mzuri zaidi ya yule asiyekuwa na ujuzi.
Mfano mtu ambae hana ujuzi wa kuendesha gari akalichuka na akaenda nalo barabarani ni nini kitakachompata huko? Atapata ajali/kusababisha ajali ambayo inaweza kusababisha kifo chake na kwa wengine pia. Kwa sababu hana ujuzi wa kuendesha gari…
Sasa mfano huo ni Sawa sawa na hawa watu ambao wanania zao na makusudio yao wemyewe ndani ya mioyo yao wala hawana ile nia ya Kristo ambao wanalenga kufanya kazi ya Mungu kwa sababu ya tamaa zao au wanasema wanamtumikia Mungu lakini hawataki kabisa kutii kile Mungu anawaambia..
Je! Huo ujuzi wa kweli ni upi unaozungumziwa na mtu anaotakiwa kuufahamu.??
Ujuzi wa kweli ni UTAKATIFU mtu yeyote aliezaliwa mara ya pili na amemaanisha kweli kumfata Yesu Kristo. Mtu huyo huufikia ujuzi wa kweli kwa kuishi maisha matakatifu na kutafuta sana kuwa Mkamilifu na mwisho wa siku anakuwa ni mkamilifu mbele za Mungu..
Tunalithibitisha hili katika maandiko..
Tito 1:1
[1]Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ‘ujuzi wa kweli’ ile iletayo utauwa;
Unaona hapo anasema …. NA UJUZI WA KWELI ULETAO UTAUWA.” kumbe ni lazima ujuzi wa kweli ulete utauwa Haleluya..
Ukiona hakuna utauwa basi bado huo sio ujuzi wa kweli..
Sasa watu hawa walikuwa na mfano wa utauwa lakini walizikana nguvu za Mungu.. matendo/mwenendo wao sio mzuri.
watu wa namna hii wana Theorogia nyingi vichwani mwao, wamesoma wanakaa usiku na mchana wakiyatafakari na kuyachambua maandiko ili yawathibitishie nia zao ambazo ni tofauti kabisa na nia au lengo la Kristo Yesu…
Watu hawa matendo yao ni maovu hata kuyasema mbele za watu yaani wanamatendo ya gizani. Na maisha yao hayamuwakilishi/ kuchukua taswira ya Yesu Kristo.
Ndipo hapo maandiko yanatimia “…wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli”
Wanajuhudi sana ni wachambuzi wa maandiko sana, wanahubiri sana lakini matendo yao ni maovu.
Hivyo sisi pia hatuna budi kupiga mbio kwa saburi katika kuufikia ule ujuzi wa kweli ambao ni UTAUWA. Kila siku omba Roho Mtakatifu akupe kuufikia ujuzi wa kweli na kwa Jina la Yesu Kristo utaufikia usikatishwe tamaa na watu wanaozikana nguvu za Mungu.. endelea mbele Bwana atakupa kuufikia ujuzi wa kweli.
Ubarikiwe sana na Bwana Yesu.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.