Fahamu maana ya ubatizo, na ulio sahihi kimaandiko.

Maswali ya Biblia No Comments

 

Kabla hatujajua maana ya ubatizo,, kwanza fikiria ukiulizwa ‘kuzamisha ni nini’ utajibuje?

Naamini utasema ni kitendo cha kutosa kitu chochote ndani ya kimiminika bila kubakiza sehemu yoyote nje. Mfano, meli ikipata ajali na kushuka chini ya bahari basi tutasema meli imezama. Hata mtu akichukua taka na kuzitupa chini ya shimo alochimba basi tunasema kazizamisha au kazizika. Na hapa tayari tumejua maana ya neno Kuzama au kuzamisha.

Neno hili kuzamisha kwa tafsiri ya lugha ya kigiriki ni BAPTIZO lakini pia kwa lugha ya kingereza tafsiri yake ni IMMERSION hivyo neno hili linaweza kutafsiriwa kwa lugha tofauti tofauti, mfano neno kanisa likitafsiriwa kwa lugha ya kingereza ni church. Mtu anaweza kusema naenda chachi akiwa na maana anaenda kanisani japokuwa neno ‘chachi’ sio lugha fasaha ya kiswahili wala kingereza lakini kwa kusema hivyo utapata kuelewa amemaanisha nini.

Hivyo basi mtu akisema amebatizwa kwenye maji maana yake amezamishwa ndani ya maji, kwa hiyo anakuwa ametumia neno la kigiriki lakini bado ataeleweka amemaanisha nini. Mtu aliyenyunyiziwa maji hajabatizwa bado maana kubatizwa ni kuzamishwa kabsa ndani ya maji, na hii ndiyo maana halisi ya ubatizo.

TURUDI KATIKA IMANI YA KIKRISTO

Katika imani ya Kikristo kuna mambo yanafanyika kama ishara lakini yana maana kubwa sana katika ulimwengu wa roho. Bwana Yesu alituagiza tushiriki meza ya Bwana yaani tule mkate na kunywa divai, tendo hili ni la kimwili lakini katika ulimwengu wa roho tunapokula mkate huo ni sawa na kuula mwili wa Kristo na tunapokunywa divai ni sawa na kunywa damu ya Yesu. Na Yesu akasema mtu asipofanya hivyo basi hana uzima ndani yake.

Yohana 6:53 “Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu”.

Tunaona hapo ni agizo la kula na kunywa chakula cha kimwili lakini ni la muhimu sana katika ulimwengu wa roho, sio jambo la mzaha hata kidogo, tena hajasema tuonje bali tuule.

Lakini pia yapo maagizo mengi ambayo Bwana Yesu aliyatoa ikiwa ni pamoja na watu kuzamishwa ndani ya maji kwa jina lake yaani ‘kubatizwa’. Tendo hili pia linafanyika katika mwili lakini katika ulimwengu wa roho linamaanisha kufa na kufufuka pamoja nae.

Wakolosai 2:12 “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu”.

Kwa hiyo mtu asipobatizwa yaani kuzamishwa katika maji bado hajapitia hatua ya kufa na kufufuka pamoja na Bwana Yesu, yeye si wa Kristo. Hata wale walionyunyiziwa maji bila kuzamishwa hao pia hawajabatizwa bado wanatakiwa wabatizwe kwa maji mengi maana hiyo ndiyo maana ya ubatizo.

Lakini kuna maswali machache ya kujiuliza
Ikiwa mtu kanyinyiziwa maji na hajabatizwa katika maji mengi, mtu huyo hawezi kwenda mbinguni? Ikiwa hawezi kwenda mbinguni inakuwaje yule mwizi aliyesulubiwa na Bwana Yesu msalabani mbona aliokolewa bila kubatizwa? Inakuwaje kuhusu Musa, Eliya mbona wao pia hawakubatizwa? Majibu ya maswali haya tutafute kwa namba zetu hapo chini tukutumie somo..

Hivyo mpendwa usidharau kabisa swala la ubatizo, ikiwa bado hujaelewa ubatizo ni nini na muhimu wake basi nakuomba tenga muda wa kutosha rudia kusoma tena taratibu lakini pia muombe Roho mtakatifu akufunulie, Na tena kwa mtu wa kusoma biblia yako na utapata majibu.

Kumbuka ubatizo sahihi ni ule unaotumia jina la Yesu kulingana na vifungu hivi
Matendo 2:38, 8:16, 10:48 na 19:5.

Kama hujampokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako muda ni sasa. Kristo yupo karibu kuchukua walio wake, mlango wa neema bado upo wazi ingia sasa kabla mlango haujafungwa, Yesu anakupenda tena anataka akupe raha kama utamkubali kama neno lake linavyosema, Mathayo 11:28-30

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *