Naomba kufahamu, kama hujabatizwa sahihi, je huwezi kuwa na Roho Mtakatifu?

Maswali ya Biblia No Comments

 

Je mtu akiwa hana ubatizo sahihi, hawezi kuwa na Roho Mtakatifu?

JIBU,

Kwanza kabisa tutambue jinsi Roho Mtakatifu anavyofanya kazi, Mungu anapomtafuta mtu mwenye dhambi humtuma Roho Mtakatifu kwenda kumshawishi mtu huyo na hapo ndipo mtu huanza kusikia hatia moyoni mwake na kisha huamua kutubu. Kwa hiyo Roho Mtakatifu hufanya kazi ya kumshawishi mtu tena hutembea nae kama rafiki yake japo anakuwa hajaingia na kuweka makao ndani yake,

Ni sawa na mwanaume ambae yupo kwenye harakati za kumchumbia mwanamke huwa anakuwa karibu nae, humpa zawadi, huongea nae maneno mazuri na kumuonyesha upendo n.k wakati anafanya hayo yote ili kumvuta mwanamke huyo anakuwa hawaja mali yake hadi pale mwanamke huyo atakapokubali kuolewa naye ndipo atakuwa mkewe halali.

Ndivyo ilivyo kwa Roho Mtakatifu, huzungumza na mtu na kuna wakati humpa maono na mambo mengine mengi ili kumshawishi mtu huyo kuishi maisha ya wokovu japo Roho Mtakatifu anakuwa bado hajaingia ndani yake. Na hata kama mtu huyo bado atakuwa hajafanya maamuzi ya kurudi kwa Bwana basi Roho Mtakatifu ataendelea kuzungumza nae siku kwa siku hadi atakapokubali

Siku amabayo mtu huyo atakubali kutubu na kubatizwa ubatizo sahihi basi Roho Mtakatifu aliyekuwa akitembea naye ataingia na kutawala ndani yake naye atakuwa amefunga ndoa na Roho Mtakatifu kwa sababu ubatizo hutoa kibali kwa Roho Mtakatifu kuingia ndani ya mtu na kufanya makao. Neno la Mungu linasema Roho Mtakatifu ni muhuri wa Mungu, sote tunatambua muhimu wa muhuri katika barua…

Waefeso 4: 30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi”.

2Wakorintho 1: 22 “..naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu”.

Roho Mtakatifu akishaingia ndani ya mtu huanza kumfundisha mambo mengine ya kiroho na huo unakuwa mwisho wa shetani kumtumia mtu huyo kwa sababu anakuwa na kibali kutoka mbinguni cha kumilikiwa na Roho Mtakatifu, tena maandiko yanasema,

Warumi 8:9 “……Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.”

Hapa neno linamaanisha mtu yoyote amabaye hajaunganishwa na Roho Mtakatifu kwa njia ya ubatizo sahihi basi huyo si wa Mungu hata kama anazungumza na kupewa maono na Roho Mtakatifu bado atakuwa si wa Mungu.

Mtu anaweza kuuliza mbona wapo waliobatizwa ubatizo sahihi lakini bado wanaishi katika dhambi? Je wewe unaweza kumkosoa Mungu aliyetoa hayo maagizo kwamba alichoagiza hakina muhimu sana kwa ajili ya ukombozi?

Ndugu jitahidi usiangalie maisha ya wengine huwezi kujua mtu huyo alibatizwa kwa sababu zipi pengine alibatizwa kuwaridhisha watu au kwa sababu ya kufuatisha taratibu za dini au kwa faida zake binafsi, jambo la msingi ni wewe kujua muhimu wa ubatizo sahihi kwa ajili ya ukombozi wako mwenyewe.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *