fahamu maana ya (yakobo 4:9)” Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza”

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, karibu katika kuyatafakari maneno ya Me mgu yatupayo uzima ndani yetu..

Kulingana na kichwa cha somo tusome

Yakobo 4:9 “Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu”.

Si kwamba haturuhusiwi kufurahi au kushangilia, pale jambo jema linapotokea, mfano ulikuwa na ndugu yako ambaye tabia zake hazikuwa njema, alikuwa jambazi alafu mwisho wa siku umuone ametubu makosa yake na ameacha kisha amekuwa mtumishi wa Mungu, huwezi ukaacha kufurahi kisha uanze kuomboleza tena, ila hapo lazima utafurahi tu na kushangilia, sasa jambo hili mbele za Mungu si mbaya Wala si jambo ambalo amelikataza

Lakini jambo ambalo Mungu alilitaka kulingana ni kifungu hicho furaha ambayo inapaswa iwe huzuni, ni pale mtu anapofurahia dhambi pale anapofurahia kutembea na mme wa mtu au mke wa mtu, alafu awe na furaha, au ni mtu wa anasa za ulimwengu huu kisha afurahie, au ni mtu wa dhuruma alafu afurahi, sasa hizi furaha ndizo ambazo Mungu alizitaka zigeuzwe kuwa huzuni.

Kwa sababu Mungu afurahishwi na dhambi na uovu tunaoufanya mbele zake, anataka pale mtu anapoona mambo anayofanya si mema machoni pake, anatazamia kuona moyo wa toba wa kugeuka kuyaacha yale makosa na kufuata njia ambayo anataka sisi tupite ya haki na kweli, hivyo Mungu uangalia sana toba na si furaha ambayo ndani yake inashangilia uovu

Luka 6:25 “… Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia”.

Jihakiki Leo maisha yako, yatazame je mambo unayoyafurahia ni mema machoni pa Mungu, au ni machukizo mbele za Mungu, ikiwa kama unayoyafanya ni mabaya ni heri uomboleze kwa ajili ya hatima ya maisha yako, kumbuka mshahara wa dhambi ni mauti, ikiwa kama Leo unafurahia udhalimu, utalipwa kulingana na hicho ulichojiwekezea

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *