Nini maana ya Kuungama?

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno y uzima ya mwokozi wetu.

Kuungama ni kukubali au kukiri jambo wazi wazi pasipo kupindisha wala kusema uongo.

Mfano Kama mtu mwenye dhambi ambae amedhamiria kumpa maisha yake Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wake. Kwa kutoka katika giza na kuingia Nuruni huyo mtu amezikiri dhambi zake na anasehemewa sawa sawa na maandiko yanavyosema..

1Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.

Unaona hapo! Anasema Tukiziungama dhambi zetu kwa maana nyingine tunaweza kusema Kutubu maana yake mtu alietubu/kuungama dhambi zake kwa kudhamiria kuziacha kabisa. Kutubu maana yake pia ni kuacha, au kugeuka.

Sasa maandiko yanaendelea kusema…

Mathayo 3:5 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani;

6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao”.

Hivyo Mtu anaetakiwa kubatizwa ni mtu ambae tayari ameziungama dhambi zake yaani kwa kukiri kuwa yeye ni mwenye dhambi ili kuruhusu damu ya Yesu Kristo imtakase na imuweke kuwa huru kabisa.

Vivyo hivyo tunapoikiri imani yetu mbele za watu maana yake tunaiungama imani yetu. Na ndio jambo ambalo Mungu pia anatarajia kuliona kwetu.

Hata mtu anae uungama uongo maana yake anaukiri uongo kama vile mashahidi wa uongo mahakamani na manabii wa uongo pia wanaukiri uongo wa baba yao ibilisi kwa kuwadanganya watu.

Mwokozi wetu Yesu Kristo alipokuwa katika hali ya kuuwawa pale anapoulizwa na Pontio Pilato kuwa yeye ndiye Mfalme wa Wayahudi? Alikiri na kukubali kuwa ndiye kama maandiko yanavyosema…

Luka 23:3 “Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu akamwambia, Wewe wasema”…..

Unaona hapo anasema kuwa “Wewe wa Sema” maana yake ni kwamba “kama ulivyosema”

Tukisoma kwenye biblia ya kiingereza imeweka wazi zaidi..

Luke 23:3[3]So Pilate asked Him, Are You the King of the Jews? And He answered him, [It is just as] you say. [I AM.]

Unaona hapo inasema katika mabano “It is just as” you say I AM.

Maana yake “ kama jinsi ulivyosema mimi NDIYE”

Hivyo Bwana Yesu hakukana mbele ya Pilato alikubali kuwa yeye ndie Mfalme wa Wayahudi.

Kama jinsi Mtume Paulo anamwambia Timotheo

1Timotheo 6:13 “Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, ALIYEYAUNGAMA MAUNGAMO MAZURI yale mbele ya Pontio Pilato,

14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo”

Hivyo popote tunapokuwa tujitambue sisi ni wakina na nani kwa kukiri imani yetu yaani kumkiri Bwana Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wetu. Pasipo kuangalia jambo lolote lile..

Haijalishi ni nani aliekombele yetu hata kama kifo kiko mbele yetu tuikiri Imani Yetu ya Kikristo kama Bwana Yesu.

Hivyo kumbuka huwezi kuikiri imani pasipo kuwa ni muombaji na msomaji wa neno na pasipo neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Maana hakuna awezae kukiri imani pasipo kuwezeshwa na Roho Mtakatifu hivyo omba sana sana Bwana azidi kukuomgezea neema ya kuikiri imani popote uendapo na popote ulipo.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *