Shalom karibu tena katika kujifunza neno la Mungu.
Maana halisi ya mstari huu, hapa Ayubu alikuwa anazungumzia watu ambao wana tabia ya kuwaonea wahitaji mfano, mayatima na wajane
Tusome
Ayubu 24:2 “Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.
3 Humfukuza punda wake asiye baba, Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.”.
Tunaona hapa kwenye mstari wa pili, Ayubu analizungumzia kundi hili namna lilivyo katiri na wala halina huruma , katika makundi haya maana hufikia hata kipindi wanaamua kabisa kuondoa alama za mipaka.
mfano unakuta, watoto waliachiwa urithi na wazazi wao labda nyumba, mashamba , viwanja nk. Lakini kwa ulafi wa ndugu unakuta wanaamua kufanya udanganyifu tu ili wawaibie haki yako, pasipo kufikiria kuwa wale ni wahitaji na wanatakiwa kuhudumiwa, na kuangalia vyema, ndiyo maana hapo akasema
Ayubu 24:2 “Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha.
Ukisoma pia sura ya tatu
3 Humfukuza punda wake asiye baba, Humtwaa rehani ng’ombe wake mwanamke mjane.”.
Wakati mwingine hufikia hata hatua ya kuwanyanyapaa wajane walifiwa na waume zao, mda mwingine unakuta hawana hata nguvu za kufanya kazi lakini unakuta labda kutokana na ugumu wa maisha inawapelekea kuchukua mikopo, lakini kwa taama za mali wale wanaowakopesha, huweka vitu vyao rehani ili watakapo shidwa kulipa wachukue vitu vyao, sasa jambo hili kiuhalisia kabisa mbele za Mungu si njema na Mungu anachukia, maana walipaswa kuhurumia kutoka na hali waliyonayo
Kutoka 22: 22 “Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.
23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima”.
Basi tukiyajua haya hatuna budi kiyatimiza yatupayo , naamini katika jamii zetu, na watu wetu wa karibu tunaoishi nao, kuna makundi haya, hivyo yatusapa kuishi nao kwa Upendo na kuwajali nyakati zote .
Zaburi 41:1
1Heri amkumbukaye mnyonge;
BWANA atamwokoa siku ya taabu.
Ubarikiwe na Bwana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.