Fahamu tofauti kati ya “Mola” na Mungu

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Mwokozi wetu libarikiwe karibu tena tujifunze neno la Mungu lililo taa ya miguu yetu

Kumekuwa na maswali mengi juu ya jina hili “Mola” limeonekana kuwa likitumiwa na watu fulani, wa imani fulani tu, lakini huwezi kuta limetumika mara nyingi katika Imani nyingine mara nyingi utakuta wakitumia jina la Mungu tu.

Je kutumia Jina “Mola” ni makosa

Kwanza kabisa maana ya Neno Mola ni MUNGU MTAWALA

Tusome baadhi ya maandiko

Ufunuo 6:10 “Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, EE MOLA, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi”.

Yuda 1:4 “Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake MOLA, na Bwana wetu Yesu Kristo”.

Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, MOLA, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo”

Kutumia Jina la Mola katika maombi au kufundisha hakuna shida kwa sababu Hilo ni jina la Mungu ambalo Lina mtambulisha Mungu kuwa Yeye ndiye anayetawala ulimwengu, anayetawala Kila kitu kilicho ijaza Dunia hii

Zaburi 24:1

Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA,

Dunia na wote wakaao ndani yake.

Lakini maana ya Jina Mungu, ni MUNGU MUUMBAJI

Yeye Mungu ndiye MUUMBAJI wa kila kitu hapa Dunia, kwa hiyo linaonyesha nani aliyetengeneza Dunia hii.

Kwahiyo haya yote ni majina ya Mungu ambayo yanapaswa yatumike na watu wote, kwa sababu yanatambulisha vyeo alivyo navyo Mungu wetu, tofauti na mtu anayeishia tu kusema Mungu tu katika maombi yake, lakini yule anayezama zaidi katika kutaja vyeo vya Mungu katika maombi yake, lazima maombi yake yatakuwa na nguvu

Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;

25 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?

31 HATA WALIPOKWISHA KUMWOMBA MUNGU, MAHALI PALE WALIPOKUSANYIKA PAKATIKISWA, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU, WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI”.

Ni vizuri kujua majina ya Mungu na vyeo vyake na maana zake ili tunapokuwa katika kuomba inakuwa inatupa nguvu zaidi ya kuomba pasipo kuchoka, maana unakuwa unamuelewa Mungu ni kwako na anatenda nini kwako

 

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *