Mtu amlindaye mwanawali wake ni mtu wa namna gani?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom mwana wa Mungu karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa mwokozi wetu Yesu Kristo.

Maandiko yanasema…

“1Wakorintho 7:34 “Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.

35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.

36 Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.

37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.

38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.”

Mtume Paulo hapa amefafanua zaidi kwa Habari ya kuoa na kutolewa ambapo alisema “ni Heri mtu akae bila kuoa kabisa, au kutoolewa kabisa kwa ajili ya Bwana, kuliko kuoa au kuolewa”hapa haijazuiliwa Moja kwa Moja bali kuna chaguzi mbili ambazo mtu anaweza kuchagua ambapo ukiolewa inamaana kuwa hautapata muda mwingi sana wa kumtumikia Bwana kwakuwa kuna wakati utakuwa nyumbani na shughuli za kifamilia tofauti na yule mtu ambaye hajaoa au kuolewa ni kwamba huyu atapata muda mwingi zaidi wa kumtumikia Mungu kwakuwa hana majukumu mengi yakumfanya akose muda na Mungu bali huyu atakuwa na uhuru mkubwa sana kiasi kwamba muda wowote anapohitaji kufanya maombi au jambo lolote linalohusiana nu Mungu anao uwezo wa kufanya hivyo na zaidi. Neno la Bwana linasema

1Wakorintho 7:32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”

Neno la Bwana linatuonyesha kuwa msingi mkubwa na Bora ni kulea mtoto katika njia Bora itakayompa uhuru wa kumtumikia Mungu pasipo kubanwa na familia na njia hiyo ni kutokuoa au kuyokuolewa(ijapokuwa katika haya yote kuoa au kutokuelewa si kila mtu anaweza kuchukuliana nalo. Wapo waliozaliwa kwa ajili ya hivyo na wanaotqka kuwa hivyo wakiwezeshwa na Munguna wasioweza kabisa. Hivyo ni jukumu la Mtu kuamgalia ikiwa anaweza au hawezi).

kwa upande mwingine ni kwamba mtu akipendezwa na kuoa au kuolewa anaweza kufanya hivyo kwakuwa haimzuilii chochote na anaweza akaupangilia huo muda alionao na akamtumikia Bwana kwa uaminifu. Neno la Bwana linasema.

1Wakorintho 7:36 “Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.

37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.

38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema

Hivyo ni vizuri kuwawekea watoto msingi wa kutokuoa na kutokuolewa kwa lengo la kumtumikia Mungu na kujitoa miwili yao kuwa dhabihu kwa Bwana ambapo ndipo wanapoweza kupata thawabu kubwa itokayo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.neno la Bwana linasema.

1Timotheo 2:7 “Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli”.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *