Shalom mwana wa Mungu muumbaji wa vyote karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Yerusalemu maana yake ni mji wa amani ambapo ndiyo mahali penye msingi wa Imani yetu.
Mji huu wa yerusalemu kabla haujapata sifa hii ya amani ulikuwa ukiitwa mji wa wakanaani kipindi ambacho wayahudi walikuwa hawajaimiliki nchi yao ambapo pia mji huu uliitwa wa wayebusi.
Wana wa Israeli walipoiteka nchi ya kanaani eneo lililokuwepo mji huu liligawanywa kwa kabila ya yuda ambapo wayebusi hawakuondolewa katika mji wa yerusalemu bali waliendelea kuumiliki mji huo.
Daudi alipoadhimia kumjengea Bwana hekalu na aliweka agano ingawa hakuruhusiwa na Mungu amjengee kwakuwa kwa sababu ya maovu na umwagaji wa damu
Hivyo Mungu akamteua Sulemani amjengee madhabahu
Pia mji ule utakaoshuka kutoka Mbinguni ambao Mungu ametuandalia mji uitwao YERUSALEMU MPYA hivyo inatupasa kuishi maisha ya utakatifu ili tuweze kuishi humo pamoja na Mungu wetu.
Hivyo Muumba wetu atakapokuja kutuchukua kwenda Mbinguni anasema huko hakitaingia kitu kinyonge bali huko wataingia wale wamchao Bwana kwa uaminifu.
Ndani ya mji huo utakaoshuka kutoka Mbinguni ambamo watakaa wale wote walioshinda na kuifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu kutakuwa na mambo ambayo hata tukiambiwa kwa sasa hayawezi kukaa katika fahamu zetu yako mambo mazuri ambayo Mungu ametuandalia wateule wake ambavyo hakuna jicho lililowahi kuona Wala sikio kusikia hivyo ili tufike huko inatupasa kuishi maisha Matakatifu.
Maandiko yanasema…
Waebrania 11:9 “Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
10 Maana alikuwa AKIUTAZAMIA MJI WENYE MISINGI, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu”.
Pia neno la Bwana linasema
Ufunuo 21:1 “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Hivyo inatupasa tutende mema na kutenda kazi ya Mungu kwa bidii ili tuwe sehemu ya wale watakaomlaki na kumtukuza Bwana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.