Beelzebuli ni nani kibiblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom karibu tujifunze maneno ya uzima yatokayo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kulingana na neno la Bwana kutoka katika maandiko haya

Mathayo 12:24

[24]Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.

Hivyo maana ya beelzebuli ni mkuu wa Pepo pia tujifunze zaidi katika neno hili la Mungu ili tupate maana zaidi.

Mathayo 9:34

[34]Lakini Mafarisayo wakasema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo.

Pia tusome maandiko haya ili tupate kuelewa zaidi ya hivi vifungu tulivyonavyo.

Mathayo 12:22 “Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.

23 Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi?

24 Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa BEELZEBULI MKUU WA PEPO”

Biblia imemtaja shetani kuwa ndiye mkuu wa ufalme wa Giza na ndiye mkuu wa Pepo waliomwasi Bwana baada ya kupingana naye na kutaka kufanana na Mungu.

Neno la Bwana linasema hivi

Luka 10:18

[18]Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.

Mafarisayo walimuonea Mungu wivu kuona mapepo yana mtii wakasema anatoa Pepo kwa kupitia beelzebuli hivyo tusiwe na wivu. Yesu alisema hivi kwamba shetani hawezi kumtoa shetani.

Neno la Bwana linasema

Mathayo 12:26 “NA SHETANI AKIMTOA SHETANI, AMEFITINIKA JUU YA NAFSI YAKE; BASI UFALME WAKE UTASIMAMAJE?

27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.

28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajili”

Pia tujifunze zaidi katika neno hili

Luka 11:14

[14]Naye alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu

 

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *