Fahamu maana ya mstari huu Zaburi 125:3 “ Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki;

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la mwokozi litukuzwe karibu katika kujifunza

Hapo aliposema fimbo ya udhalimu haitakaa juu ya fungu la mwenye haki

Turejee

Zaburi 125:2-3
[2]Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,
Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,
Tangu sasa na hata milele.

[3]Kwa maana fimbo ya udhalimu
Haitakaa juu ya fungu la wenye haki;
Wenye haki wasije wakainyosha
Mikono yao kwenye upotovu.

Maandiko haya yanaeleza wazi, jambo ambalo Mungu analitenda kwa watoto wake haswa wale wanaotiii sheria ya Mungu (Watakatifu) watu kama hawa Mungu amewahakikishia ulinzi, na baraka na kuwaepusha na uharibu

Jambo hili tunaliona katika habari ya lutu, baada ya Mungu kuona nchi ya sodoma imezii uovu na machafu, ilimfabya Mungu alichime mji huo kwa moto na kibariti ila kwa sababu ndani ya mji huo kulikuwa na wenye haki wake, aliwaepusha na jambo hilo

Mwanzo 19:14-17

[14]Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze.

[15]Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu.

[16]Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi BWANA alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji.

[17]Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.

Lakini pia hapo aliposema

Wenye haki wasije wakainyosha
Mikono yao kwenye upotovu

Alitoa msisitizo kwa wenye haki akiwa nao wataelekea mambo ya ulimwengu huu watadondokea kazi hasira ya Mungu, ndiyo maana kuna umuhimu mkubwa wa kumpokea Yesu Kristo maana yaye anatupa nguvu ya kushinda dhambi

Ni jukumu letu siku zote kuthamini kazi ya Mungu na wema wake kwetu kwa kujiepusha na maovu ili tusipotelee katika uovu tena

Ubarikiwe…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *