Mwanamke jitambue na ujithamini.

Mwanamke No Comments

Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo karibu tujifunze  Neno la uzima.

Somo hili ni maalumu kwa wanawake wote waliomwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yao(Wanaoukiri uchaji wa Mungu). Hivyo ikiwa wewe ni mwanamke ni muhimu sana ukasoma na kutafakari ujumbe huu na Yesu Kristo atasema na wewe kwa namna nyingine zaidi.

Katika nyakati hizi za mwisho shetani anafanya kazi kwa kasi sana kuhakikisha anaharibu mahusiano yaliyopo kati ya Mungu na waamini. Na jambo hili ameshalifanikisha kwa kiasi kikubwa sana. Hasa kafanikisha kuwapofusha macho wanawake wa Kristo na kuiacha asili yao yaani mwenendo wanaotakiwa kuwa nao kama kanisa la Kristo.

Hebu tusome mstari mmoja na katika huo tutajifunza kitu kingine kikubwa sana.

Mathayo 5:27-28”

[27] Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;

[28]lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Umewahi kuutafakari kwa kina mstari huu? Kwa nini anasema kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye? Na kwa nini Bwana Yesu hakusema pia katika upande wa wanaume? Kwa nini pia hakusema “ NA KILA MWANAMKE  AMTAZAMAYE MWANAUME KWA KUMTAMANI AMESHAKWISHA KUZINI NAYE  PIA”?

Ni kwa nini katika mstari huu tunaona anaelengwa zaidi ni mwanamke juu ya kutamanika na sio mwanamume? Ni jambo la kutafakari sana.

Kwa kawaida na ndivyo Mungu alivyotaka(alivyoumba jinsia moja inatamanika zaidi kuliko nyingine) iwe ni kwamba mwili wa mwanamke umeumbwa kwa jinsi ya kutamanika, yaani asili ya maumbile yake ni ya kutamanika/kuvutia kwa watu wenye jinsia ya kiume. hili ni jambo la kiasili kabisa ambalo Mungu ameruhusu liwepo na lina maana kubwa sana.

Na ndio maana maandiko yanasema..

1 Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na Wajipambe KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na adabu nzuri, na moyowa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;”

maandiko yanamtaka mwanamke avae nguo zinazo  mstiri mwili wake. Leo hii kumekuwa na idadi kubwa ya Wanawake wa Kikristo wanaovaa nguo zisizositiri maumbile yao. Leo hii utakuta mwanamke anaesema amejazwa Roho anavaa suruali tena zinazombana mapaja yake yanaonekana wazi wazi, makalio vivyo hivyo.

Tambua mapaja,miguu yako anayetakiwa kuyaona ni Mume wako tu na si kila mtu aone jinsi ulivyo unamkosea heshima Roho Mtakatifu alie ndani yako. kuanzia chini kidogo ya magoti mpaka kwenye kifua kwa mwanamke hizo zote ni sehemu za siri na ni lazima zifunikwe na mavazi ya kujisitiri. Ndio maana mwanamke hata kwa asili huwezi kutembea kifua wazi.

Ujali mwili wako na kuuthamini wewe dada unaeimba kwaya, na wewe mshirika acha kuvaa nguo fupi na suruali uwapo  nje na kanisa kumbuka mwili wako huo ni hekalu la Roho wa Mungu anaekaa ndani yako.

Ni nani aliekudanganya ukivaa hivyo ndio fasheni na staili mpya? Na ndio maana inakuwa rahisi kuanguka katika dhambi maana milango unaifungua mwenyewe na mapepo kuingia ndani yako(maana watu wengi wanakutazama jinsi ulivyo na wanazini na wewe pasipo hata kujua). lakini leo hii wanawake wakiambiwa makanisani kuvaa mavazi ya kujisitiri nyuso zinabadilika hata kama walikuwa na furaha “utasikia tuneokolewa kwa neema, tunaishi katika neema si vitu vya kujali sana anataka kuleta tu sheria zake hatuko kipindi cha torati nk“wanachukia.. sikiliza wewe dada,mama kama kingelikuwa ni kitu kizuri hata usingekasirika lakini unapoambiwa ukweli na kwa faida yako unanuna..

Ewe mwanamke usiifatishe namna ya ulimwengu huu kumbuka wewe ni chumvi ya ulimwengu watu wanajifunza kutoka kwako, wanakutazama wewe ni kama Barua ya Kristo inayosomwa na kila mtu, leo hii unapotembea njiani ni ngumu hata watu kutambua kama wewe ni mkristo wanakuona kama mtu wa mataifa tu kutokana na jinsi ulivyo.

Hayo mawigi unamvalia nani? Hizo suruali unamvalia nani? Kucha bandia unamuwekea nani? Lipstick na make-ups unampakia nani? Hakuna mwanaume mwenye Roho wa Mungu anataka kuoa mwanamke wa namna hii. Na ni machukizo kwa Mungu acha.

Muonekano wako hauna tofauti na watu wa mataifa, unavaa suruali,nguo fupi,unapaka make-ups,unaweka kucha za bandia, unaweka rasta kichwani kwako, unavaa mawigi na kupaka kucha zako rangi,ukiwa mtaani/Beach unavaa vitop, nk

na usema umeokolewa dada,mama, ikiwa unasema umeokolewa IKO WAPI NGUVU YA MSALABA?  inayowabadilisha watu kuanzia tabia mpaka mwenendo nao wanafanania Kristo? ikiwa umeokolewa kweli kweli wewe dada,wewe mama,mke wa mchungaji nk ni lazima badiliko litatokea ndani yako likianzia ndani na kudhirika nje.

Maandiko yanasema…

Mhubiri 7:29” Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi”

Mungu kakuumba mkamilifu baki katika asili yako Mungu asingeshindwa kukuumba na makucha mengine kama unayoweka sasa yakawa yanaota juu yake, wala asingeshindwa kukuumba na nywele nyingine juu hapo kama unazosuka(Rasta).. wala asingeshindwa kabisa kukuumba na kucha zinazobadilika badilika rangi kila siku.. ikiwa ameweza kumuumba kinyonga anaebadilika rangi mwili mzima kama jinsi atakavyo angeshidwa nini kukuumba na makucha na make-ups na lipstick zinazobadilika badilika kama jinsi utakavyo? Huoni kama ni jmbo dogo hilo kwake?

Mungu anakusudi lake kukuumba hivyo acha kumsahihisha.. badilika leo acha kuvaa nguo zisizositiri mwili wako anza kujitambua na badilika unayoyafanya sasa yatakugharimu baadae kila unachokifanya kina matokeo hata kama huyaoni kwa sasa.

Ubarikiwe sana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *