Neno hili linatoka katika maneno haya ya Mungu.
Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”
Kutokana na haya maandiko tunaona utajiri aliouzungumzia kristo ni utajiri mwingine tofauti na utajiri wa pesa, magari, nyumba na zaidi ambapo ni utajiri huu wa mwitikio wa wokovu ndani ya mtu neno linasema.
Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani”.
Ambapo tunaona kuna maskini wa pesa, magari, na majumba ambao ni matajiri rohoni. Ambapo pia kuna wengine walio matajiri wa magari, majumba, fedha na zaidi huku wakiwa na amani, furaha, ushindi tele toka kwa Bwana ambapo mtu wa kidunia akifanikiwa unakuta anatumia nguvu za Giza kupata utajiri ambao mwisho wake huwa ni mateso na mahangaiko kwakuwa unakuta huo utajiri ulihusisha umwagaji wa damu za watu ambapo huleta majuto naateso tuu Kila siku.
Hivyo inatupasa kumfuata Yesu kwakuwa alisema kuwa tuutafute ufalme wa Mbinguni kwanza ndipo MENGINE tutazidishiwa na yeye hivyo katika kuishi maisha ya utakatifu na kumtumikia Mungu baraka zote zitamiminika maishani mwako na utaufurahia wokovu sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.