Neno hili linamaanisha kuwa ni mtu wa kwanza kuumbwa na Mungu katika asili ya udongo na baada ya kupuliziwa pumzi ya Bwana akaweza kutolewa mwanadamu wa kwanza mwenye uhai na ndiye huyu aitwaye Adamu.
Tukiangalia maandiko ya Bwana wetu Yesu Kristo maneno yake ya uzima yanasema hivi.
Mwanzo 2:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai”.
Na Mungu aliweza kuwapatia wote wawili jina hili la Adamu yaani mwañamke na mwanaume baada ya Yesu kuwaumba nakuwatamkia baraka za maisha yao.
Hata sisi tunalitumia jina hili kwakuwa sisi asili yetu ni udongo na tuliumbwa kwa udongo ndiyo maana wakati wa kufa tunazikwa ardhini pekee tukimaanisha kuwa ndiyo asili yetu udongo.
Baada ya kushinda vita vyote vya hapa duniani tutakutana na mwokozi wetu Yesu Kristo huko Mbinguni tutaitwa Wana wa Mungu aliye hai ambapo hatutaitwa Wana wa Adamu bali ni Wana wa Mungu kwakuwa tutapewa miili mipya.
Neno la Bwana linasema hivi
Marko 12:25 “Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni”.
JE? Tunalotamani kuwa tunaweza kuweka miili mipya itokayo kwa kristo? Jibu ni ndiyo kwakuwa Neema hii tunaweza ipata tukiwa ndani ya Kristo pekee yaani kwa kumkiri Yeye ni Bwana na mwokozi wa maisha yetu.hivyo inatupasa kumgeukia Bwana kwa kuyavua matendo ya kale na kutenda mapya kwakuwa yeye ndiye kimbilio la wengi.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.