Lipa gharama hizi ukitaka kumjua Mungu.*
Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo Karibu tuyatafakari maneno ya uzima.
Ikiwa umemuamini Yesu Kristo ni lazima kuna gharama lazima uzilipe ili kumuelewa zaidi vinginevyo hutamuelewa kabisa hata kidogo na utaendelea kuwa mtu wa kawaida kabisa siku baada ya siku na mpaka unakufa.
Watu wengi wanatamani kumjua Mungu kweli lakini hawataki kulipa gharama hivyo wanaishia kutamani na kubaki hivyo hivyo tu..
Zipo gharama kuu tatu zipo nyingi lakini hizi ndio kuu ambazo ukifanikiwa basi utaanza kumuelewa Mungu.
1# Gharama ya namba 01: Soma Neno na kuomba.
Hii ni gharama ambayo kila Mkristo ni lazima aingie ili aweze kumuelewa Mungu.
Maombi sio karama, wala kusoma neno sio karama bali ni kwa kila Mkristo, “ _kuomba ni kazi lakini ndio njia ambayo unapaswa kuifata_ ” pia kusoma neno ili umuelewe Mungu ni lazima usome neno na si kusoma tu lazima ulitafakari(Yoshua 1:9) na kulitendea kazi.
Wakristo wengi ni rahisi kukaa na kuangalia tamthilia,kuongea na marafiki au jamaa,nk kwa muda wa zaidi hata ya masaa 3 au 4 lakini ukiwaambia kusoma neno na kuomba hata wanapoingia kwenye maombi na kusoma neno utaona wanaanza kupiga miayo na usingizi ndugu “huwezi kumjua Mungu/kumuelewa Mungu kwa namna hiyo”
Mitume walifanikiwa kumjua Yesu zaidi si kwamba kwa sababu Mungu aliwapendelea na kuwaona wa kipekee tunaposoma nyaraka tunafikiri kwamba walikuwa wanakaa tu Mungu anawapa mafundisho ya kuwafundisha watu la.! Maandiko yanasema..
Matendo ya Mitume 6:4
“na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.”
Unaona hapo? Maana yake hakikuwa kuti cha siku moja moja lakini yalikuwa maisha yao ya kila siku na ndio maana wakafanikiwa kumuelewa zaidi Mungu.
Wakolosai 4:12
“Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.”
_Maombi ni bidii(maombi na pumzi ya mtu aliezaliwa mara ya pili na neno ni chakula cha mtu aliezaliwa mara ya pili)_ pasipo hivi mtu wa ndani hatakuwa na nguvu na hutaweza kumuelewa Mungu.
Watu waliokaa kwa muda mrefu katika imani lakini hawasomi neno hawaombi siku zote wanabaki pale pale tu miaka yote wataanza kujisifia “ _nimekaa kwenye wokovu miaka 30 au 20 nk”_ tatizo si kukaa katika wokovu kwa miaka mingi je kuna maendeleo katika wokovu wako,?. Ni kipi umekifanya?
Ikiwa umedhamiria kweli kumfata Kristo Lipa gharama hii..
#2 Gharama namba 02: Utakatifu/usafi.
Hii ni gharama ambayo ni lazima unatakiwa kuilipa.
Huwezi kumuelewa Mungu ikiwa unaishi maisha ya dhambi, au kuanguka anguka dhambini ni ngumu. Yaani mtindo wako wa maisha umezoelea dhambi tu kisa utatubu ndugu.. beba gharama hii..
Yapo mafundisho manyonge(ya watoto) ambayo watu wanafundishwa kwamba “ _hata ukianguka dhambini ukiomba rehema Mungu atakusamehe/utasamehewa tuko chini ya neema”_ ndugu nataka nikwambie haya ni mafundisho ya awali ya watoto kabisa na hutakiwi kuendana nayo.. kweli utasamehewa lakini unaonekana ni mtoto.
Hebu tutafakari mstari huu tutapata kitu kikubwa sana..
1 Yohana 2:1
“Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,”
Umewahi kufikiri kwa nini Yohana anasema jambo hili?
Ni kwa sababu mtoto siku zote uelewa wake ni mdogo yaani anakosea kosea mara kwa mara(simaanishi kwamba hatukosei la!) Lakini kwa sababu ya uchanga wake na kukosa uelewa mkubwa anakuwa ni mtu wa kukosea kosea na ni mtu wa kuomba msamaha mara kwa mara kwa kosa lile lile analolirudia kulifanya leo kazini kaomba msamaha baada ya mwezi kazini tena anarudi kuomba msamaha hii ni hatua ya utoto.
Lazima ukue utoke katika utoto uende katika hatua ya ujana maandiko yanasema..
1 Yohana 2:14
“Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.”
Unaona hapo 14b? “…. _nimewaandikia ninyi vijana,kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu,nanyi mmemshinda yule mwovu.”_
Nataka utafakari hapa sifa za kijana “ _ana nguvu, neno la Mungu linakaa ndani yake, n amemshinda mwovu”_ hii ni hali ya juu ya ukomavu ya kumjua Mungu, ukiwa na nguvu na neno la Mungu liko ndani yako maana yake lazima ibilisi utamshinda tu kwa namna yoyote kwa sababu kivyovyote atakavyokuja nguvu na neno viko ndani yako lazima utamshinda.
Mfano mzuri watafakari Mitume, ukisoma kitabu cha matendo ya Mitume au nyaraka za mitume hutaona mahali fulani Paulo ameenda labda Efeso kahubiri kaenda antiokia kaanguka dhambini nk hutaona mahali popote biblia inaonyesha mitume kuna mahali walikuwa wanaanguka dhambini bali walikuwa imara.
Si kwa sababu biblia imeficha maovu yao kwa sababu wao ni Mitume la! Bali ni kwa sababu walikuwa na nguvu, neno linakaa ndani yao hata wakafanikiwa kumshinda shetani katika kila eneo na kuupindua ulimwengu.
Ikiwa unaishi mtindo fulani wa maisha unaoeleza dhambi ndugu hutaona hata uwepo wa Mungu kabisa acha maisha ya kuzoeleaa dhambi anza kupiga hatua utakatifu.
“ Usizoelee dhambi na ukafiri kila mtu yuko kama wewe la! Si kila mtu anatenda dhambi au kuzoelea dhambi wapo watu wanaoishi maisha yanayompendeza Mungu na kila siku wanapiga hatua”
Maandiko yanasema na alie msafi azidi kujitakasa na mchafu azidi kuwa mchafu maana yake kuna watu ni wasafi(wanaishi maisha ya utakatifu na wanazidi sana katika kufanya hivyo).
Mmoja wapo nimekuombea uwe ni wewe. Usijitumainishe kwamba wote tunatenda dhambi.. tunazini,kusema uongo,kuiba,kula rushwa,kuangalia picha za uchi nk, ndugu wapo watu hawafanyi yote hayo maisha yao yote wanazidi kuwa wasafi.
2 Timotheo 2:21
“Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.”
Unaona hapo? “…. _Kujitakasa kwa kujitenga..”_ hasemi kutakaswa na kutengwa la!, umeshatakaswa kweli na kutengwa lakini wewe unajukumu la kujitenga na mambo yote yasiyofaa.
Ili uwe chomo kifaacho kwa kila kazi iliyo njema. Haleluya..!
Huwezi kuwa chombo kifaacho ikiwa huishi maisha matakatifu.
Kimbia tamaa za ujanani za Muda mfupi..
3# Gharama ya 03: kumtumikia Mungu.
Ukweli ni kwamba huwezi kumuelewa Mungu katika viwango vingine ikiwa hutumiki katika nyumba ya Mungu au kufanya kazi yake..
Yaani wewe huwezi kuwahubiria watu injli,huwezi kuwaombea watu,unaenda kanisani na kurudi basi.. ndugu watu wanaomfahamu Mungu wako wanawahubiria mataifa na kuwafanya kuwa wanafunzi, wanawachunga na kuhakikisha wanakua katika imani vizuri.
Huwezi kufahamu utendaji na nguvu za Mungu, na siri za Mungu ukiwa hutumiki mahali popote yaani wewe upoupo tu, si mtowaji,si muombaji,
Maandiko yanasema..
1 Wakorintho 4:1
“Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.”
Mawakiri wa siri za Mungu ni watu wanaofanya kazi ya Mungu na sio wachungaji tu hata wewe ni wakari ikiwa utataka kuwa hivyo.
Leo hii watu hawawezi kumtumikia Mungu pasipo fedha, yaani mtu kuitwa kuimba atataka kiasi fulani cha fedha, mpiga drums,keyboard hawezi kufanya hivyo bila kulipwa.. (sisemi ni vibaya kulipwa la! Lakini hatutakiwi kuweka kipaumbele bila fedha hatuwezi fanya huko si kumtumikia Mungu ipasavyo).
Mhuburi akiitwa sehemu anataka fedha yaani pesa,pesa pesa tu huko si kumtumikia Mungu ipasavyo unaenda kuwaombea watu au watu kuonana na nabii ni pesa,sijui mafuta pesa ndugu yangu huko unaibiwa..
Paulo anasema…
1 Wakorintho 9:18
“Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.”
Injili inatolewa bila gharama injili yoyote yenye gharama ni wizi.. kumuona nabii mpaka pesa(ni wapi kwenye biblia mitume walifanya hivyo)? Kwenda kuimba mahali mpaka kiasi fulani cha pesa,
Ndugu ukitaka kumuelewa Mungu zaidi ikiwa wewe ni mchungaji, unakarama ya uponyaji nk usiweke pesa mbele ikiwa utapewa sawa lakini usiweke bila pesa hufanyi.
Ubarikiwe sana.
Maranatha.
Mawasiliano:0613079530.
Kwa msaada zaidi wa kiroho piga namba hizo utasaidiwa bure kabisa.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.