Je! biblia inaturuhusu tuwe na hasira sawa sawa na Waefeso 4:26?

Maswali ya Biblia No Comments

Je! biblia inaturuhusu tuwe na hasira sawa sawa na Waefeso 4:26?

Awali ya yote tusome andiko lenyewe.

Waefeso 4:26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;

Hapo biblia inasema tuwe na hasira ila tusitende dhambi, lakini sehemu nyingine inasema hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu (Mhubiri 7:9). Hapo imekaaje?

Hasira inayozungumziwa hapo kwamba tuwe nayo lakini tusitende dhambi..ni hasira inayozalika ndani yetu pale tunapoona watu wakimdhahaki Mungu, au wakifanya mambo yasiyompendeza Mungu.. mfano hebu chukulia upo ibadani unaona watu wakifanya uasherati au wakifanya jambo lolote baya ambalo ni machukizo kwa Mungu, bila shaka kama una Roho Mtakatifu utawaka na kuwakasirikia sana hao watu. Hii ndiyo hasira inayozungumziwa hapo kwamba tuwe nayo lakini tusitende dhambi wala jua lisichwe na uchungu wetu bado hujaondoka.

Maana yake badala ya kusema maneno mabaya juu yao..tunapaswa kuwahubiria na kuwakemea watubu dhambi zao ili wasiende kuangamia motoni. Na vile vile ndugu yako amekukasirisha, usiichie tu kukasira na kumuona ndugu yako mbaya..bali muonye, mshauri, mrekebishe ili mkae katika amani.

Halikadhalika unaona watu wa kidunia wakimdhahaki Mungu na kufanya mambo yasiyostahili hata katika jamii, suluhisho sio kuwakasirikia tu. Ni kweli we kama mkristo uliyejazwa Roho Mtakatifu utakasirishwa na matendo maovu yanayoendelea ulimwenguni lakini hasira yetu inapaswa izae matunda mema (yaani tuwahubirie na kuwaombea neema ya Yesu).

Je! Umempokea Yesu ipasavyo? Tunaishi ukingoni mwa nyakati, Kristo yupo mlangoni kurudi. Hivyo kama bado hujampokea Yesu wa kweli, usiendelee kukawia kawia maana neema ya Mungu haitadumu milele kwako…unapaswa sasa kutubu dhambi zako na kumaanisha kabisa kumgeukia Yesu na kuacha ulimwengu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *