
KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE OUVU.
Jina la Bwana wa Mabwana YESU KRISTO libarikiwe daima.
Neno la Mungu linasema..
2Timotheo 2:19 “Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE OUVU.”
Kulitaja jina la Bwana ni zaidi ya kutamka kwa mdomo, ni zaidi ya kusema ”Bwana Yesu asifiwe”.
Wewe tu kusema mimi ni Mkristo, tayari umeshalitaja jina la Bwana. Na Kumbuka jina la Bwana sio “MUNGU” jina la Mungu ni YESU KRISTO. (Yohana 5:43).
Ni kama tu wewe unaitwa “Mwanadamu” lakini hilo sio jina lako. Jina lako pengine ni Paulo.
Vivyo hivyo Neno “Mungu” limetokana na neno “MUUMBA” yaani muumbaji. Lakini jina la huyo muumbaji anaitwa YEHOVA MWOKOZI (YESU KRISTO WA NAZARETHI).
Kwahiyo Mungu anaposema usilitaje jina lake bure (kutoka 20:7), hamaanishi kama tunavyotafsiri kwamba kutamka Neno hilo “MUNGU” bure au kuhusishanisha kwenye mambo yasiyo na maana ndio kulitaja jina lake bure, hapana. Anamaanisha jina lake hasa YEHOVA, ambalo kwa sasa ni YESU KRISTO. Hatupaswi kulitaja taja taja tu ovyo.
Kwanini hatupaswi kulitaja bure? Kwasababu hilo ni jina TAKATIFU SANA ambalo limebeba sifa zote za Mungu na neema ya Mungu kwa viumbe vyake.
Hata kiongozi wa nchi, huwezi tu kutaja taja jina lake ovyo, unalitaja kwa heshima na kwa sababu. Si zaidi huyu Mfalme wa Wafalme wa dunia yote na mkuu wa uzima, YESU KRISTO, MUNGU MKUU, NA MWOKOZI WETU (Tito 2:13).
Jina lake linapaswa kuheshimiwa mara nyingi sana na kuogopwa sana. Sio kila mtu anaweza kulitaja taja tu bure, kuna hatari kubwa katika kulitaja jina la Mungu bure, hata wakati mwingine mauti. Na pia kama tulivyoona, hili ni jina TAKATIFU SANA, hivyo kila alitajaye ni sharti ahakikishe ameachana na uchafu wote wa rohoni na mwilini.
Lakini utamkuta mtu hajaokoka, lakini anakiri ni ”Mkristo”, anafanya maovu yake kwa siri na bado anajihita ni Mkristo aliyeokoka, pasipo kujua kuwa analitaja jina la Bwana bure. Ndugu kama ni wewe, Neno la Mungu leo linakuonya..
“...Kila alitajaye jina la Bwana na auache ouvu.” (2Timotheo2:19).
Kumbuka anasema na AUACHE, na sio aombewe aache. Hapana, uovu unachwa na mtu mwenyewe kwa lazima.
Ili uitwe mkristo, au uweze kulitaja jina la Bwana, ni lazima uache uzinzi na uasherati kwa vitendo kabisa, ni lazima uache masengenyo, matusi, ulevi, kujishua, kujipodoa, kuvaa mavazi ya aibu, na uovu wote ni lazima UACHE. Tofauti na hapo ni heri usilitaje tena jina la Mungu bure, ni heri ubaki na upagani wako kama hutaki kuwa mkristo wa kweli.
Jina la Kristo lisitamkwe kabisa kinywani mwako kama haupo tayari kuuacha ouvu.
Jina la mwokozi wetu YESU KRISTO na lihimidiwe daima, Amina.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.