
BASI NINGOJENI ASEMA BWANA.
Sefania 3:8 “Basi ningojeni, asema Bwana, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu”.
Majira yaliyopo mbele yetu, si rafiki kabisa ndugu yangu, Bwana ameshaihidi kuharibu hii dunia na kuifanya ukiwa kama hapo mwanzo, kwasababu ya maovu yanayoendelea.
Isaya 13:6 Pigeni kelele za hofu; maana siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
[7]Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.
[8]Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
Ndugu, maovu yanayoendelea sasa hivi ni mengi sana, ni mambo yasiyotamkika yanaendelea katika hii dunia, lakini usidhani kuwa itakuwa hivi siku zote, na kwamba Bwana atavumilia daima, anasema NINGOJENI..unaelewa maana yake?
Hebu wazia umemfanyia mtu jambo baya, halafu anakupigia simu anakuambia ningoje! unadhani akifika itakuaje? bila shaka patachimbika!! (hiyo ni mfano tu wa watu kidunia).
Lakini Bwana anasema ningojeni, sasa hivi anatuvumilia.. lakini siku ya ghadhabu yake itakapofika ndipo waovu wote watalia na kusaga meno kwasababu hasira yake haitarudi mpaka atimize kusudi lake.
Yeremia 30:23 Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea tufani ya kudumu; itawaangukia waovu vichwani.
[24]Hasira kali ya BWANA haitarudi, hata atakapokwisha kutenda, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtayafahamu haya.
Ndugu, kama ulikuwa hufahamu kalenda ya Mungu, ni kwamba kwasasa hivi tunachokingojea mbele yetu ni UNYAKUO tu, dalili zote zimeshatimia, Na Unyakuo huo hautakuwa kwa watu wote, hapana bali utakuwa ni kwa watakatifu wa Bwana (Bibi-arusi wa Kristo).
Je! umefanyika mkristo wa kweli? au u miongoni mwa wakristo jina?
Kumbuka kukiri tu Kristo kwa kinywa haikutoshi kuwa mkristo wa kweli, maana hata walevi na wahuni wanaweza kukiri. Bali unapaswa uwe na mabadiliko ya kweli yanayopasa ukristo wa kweli. Lakini kama unakiri umeokoka na huku ni msengenyaji, muasherati, mtukanaji, unavaa kiulimwengu, unajipodoa kama watu wa ulimwengu huu, unashabikia mambo ya kiulimwengu, bado hujawa mkristo wa kweli, haijalishi utakiri kuwa umeokoka mara elfu!!.
Tubu leo mpe Yesu maisha yako, ukabatizwe katika ubatizo sahihi, na kupokea Roho Mtakatifu uishi maisha ya utakatifu. Huu Ulimwengu si rafiki, yasalimishe maisha yako kwa Bwana.
Isaya 13:9 Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.