Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo.
Tukisoma Mwanzo 28:21
[21]”nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.”
Katika sura hii tunaoneshwa ugumu wa safari ya Yakobo kuelekea Ugenini nchi ya Baba yake akimkimbia nduguye Esau.
Sasa alipokuwa kule jangwani peke yake pasipo msaada, Wala mtu Wala kitu chochote ndipo anaweka nadhiri kwa Mungu wake akimwambia maneno haya
‘nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu’.
Sasa swali linakuja; Je! Hakumwamini YEHOVA kama Mungu wake kabla? Mpaka pale haja yake hiyo itakapotimizwa, kama tunavyosoma yanatimia baada ya miaka 20! Kwahiyo hapo katikati ya hiyo 20 YEHOVA hakuwa Mungu wake!?
Jibu ni LA! Si kwamba Yakobo anamweka Mungu kwenye majaribio! Kwamba atimiziwe haja/nadhiri yake kwanza ndipo Amfanye kuwa Bwana Mungu kwake! Hiyo sio kweli. Na Kama ingekuwa hivyo tusingeona kipindi chote hicho akimtumainia Mungu wa Baba zake, angeendelea na vitu vingine mpaka hitaji lake Hilo likitimizwa! Lakini haikuwa hivyo, alimtumainia Mungu siku zote.
Yakobo alikuwa akiongezea tu namna kujitoa kwake kwa Mungu kungeongezeka baada ya kurudishwa salama, Ndio maana anaongezea kwa kusema atamtolea Mungu wake FUNGU la kumi kwa atakachokipata. Maana kabla hakuwa na chochote hapo kabla
Mwanzo 28
[21]”nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.
[22]Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi. “
Yaani anamwambia Mungu nitakutumikia vizuri Zaidi endapo nitarudi salama nchi ya Ugenini. Mfano Mtu anamwambia Mungu ‘ nitakutukuza endapo utaniponya ugonjwa huu’.
Kwakusema hivyo haimaanishi anamwekea Mungu masharti Bali anaonesha kile kikwazo chake, kwamba atatumika vizuri zaidi kitakapoondolewa. Na hiyo ndio Maana halisi ya Yakobo.
Ubarikiwe sana
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.