Shalom, karibu tujifunze biblia..
Tusome andiko..
[10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
JIBU
Ili tujue sababu za Yesu kumwambia wanafunzi wake maneno hayo anza kusoma mistari ya juu utaona walimuuliza swali kuhusu imani, maana walitaka awaongezee imani…
Yesu aliwajibu kwa kuwaambia kama wangekuwa na imani hata yenye kulingana na chembe ya haradani basi wangeweza kuuambia mkuyu ung’oke na ukapandwe baharini nao ungetii.
Luka 17:6
[6]Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
Yesu alimaanisha haikuwa na haja ya kuongezewa imani kwa sababu hata ile ndogo walokuwa nayo ingetosha kabsa kufanya mambo makubwa, Mitume walikuwa na hiyo imani ndogo ambayo hata sisi tunayo, lakini mitume hawakujua namna ya kuitumia.
Na Yesu anaendelea kuwaambia kwa mifano ili yafanyike mambo hayo basi walitakiwa kuwa kama watumwa wasio na faida kwa Bwana wao,tuusome mfano wenyewe.
Luka 17:7-10
[7]Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?
[8]Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?
[9Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?
[10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
Mfano huo upo wazi kabisa, zamani watu walipochukuliwa kuwa watumwa hawakuhesabiwa kama waajiriwa walichukuliwa kama wanyama mfano wa punda, kazi yao ilikuwa ni kuwatumikia bwana zao tu na si kujitafutia maisha yao wenyewe.
Yesu anatumia mfano wa mtumwa ambae amewekwa na Bwana wake awe mkulima katika shamba lake, asubuhi anaondoka kisha jioni anarudi kwa Bwana wake.
Anauliza, je atakaporudi Bwana wake atamwambia akae apumzike? Bila shaka hapana anaweza kupewa majukumu mengine ili kuhakikisha Bwana wake ametosheka sana hana uhitaji wa kitu kingine hapo ndipo na yeye atapata nafasi ya kupumzika.
Yesu aliwaambia mfano huo ili wanafunzi wapate kujua namna wanavyotakiwa kuwa mbele za Mungu.
“[10]Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.”
Alimaanisha kuwa tukihitaji kufanikisha jambo lolote la imani basi hatuna budi kuwa kama watumwa wasio na faida, tutumike kwanza bila kutarajia malipo yoyote.
Ukiwa muhubiri kwa miaka ishirini na hujaona mabadiliko yoyote katika maisha yako haina haja ya kumuuliza Bwana kwa nini iwe hivyo badala yake yakupasa uwe kama mtumwa asiye na faida. Hivyo ndivyo Bwana anavyotaka kuona tukimtumikia.
Wapo watumishi wa Mungu waliokuwa nawamtumikia Mungu wakiwa na matarajio fulani lakini hawakuyaona na warudi nyuma na wengine wameacha kabisa utumishi.
Ndugu tunapoamua kumtumikia Mungu lazima tuzijue kanuni za utumishi, ukiwa na Lengo la kunufaika na sadaka ni bora uache uelekeze nguvu zako katika kazi nyingine. Unaweza kutumika kwa muda mrefu na usipate kitu kutoka kwa Mungu je bado utaendelea kumtumikia?
Tukubali kuwa watumwa wasio na faida, kama atatupa chochote ni sawa lakini hata asipotupa ni sawa pia katika yote tutambue mawazo ya Mungu ni mazuri kwetu siku zote. Hivyo Bwana anatuambia tukiitaka imani basi tuwe watumwa wasio na faida..
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.