ENYI WAPUMBAVU, LINI MTAKAPOPATA AKILI? Zaburi 94:7 “Nao husema, BWANA haoni; Mungu wa Yakobo hafikiri. [8]Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini; Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili? Mpumbavu ni nani kibiblia? Mpumbavu ni mtu asiye na akili, na hapa hatuzungumzii akili ya darasani au kuwa na maarifa ya kidunia, hapana, unaweza ukawa na degree zote au ukawa namba ..
Category : Uncategorized
ONJENI, MWONE KUWA BWANA YU MWEMA Zaburi 34:8 Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. Ulishatembelea soko la vyakula, na kukutana na wafanya-biashara wengi, halafu kila mmoja anakuvutia upande wake ununue bidhaa yake. Kwakawaida si rahisi kuchukua maamuzi, kwa hofu ya kuuziwa kitu kusicho bora. Wafanyabiashara wengi hulijua hilo, hivyo wanachokifanya ni ..
USINIPUNGUZIE MWENDO. Tukiwa bado tupo mwanzo wa mwaka, ni wakati wa kushika sana vile tulivyo navyo na kuendelea mbele, wala si wakati wa kurudi nyuma kabisa au kupunguza mwendo uliokuwa nayo. Ulikuwa upo mbali na anasa mwaka jana, basi huu mwaka unapasawa kwenda mbali zaidi, ulikuwa umejitenga na mambo ya kiulimwengu mwaka jana, mwaka huu ..
SULIBISHA MWILI WAKO KWA BWANA. Wagalatia 5:24 “Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. [25]Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho”. Siku zote fahamu kuwa adui wa kwanza wa mtu ni MWILI wake na wala sio shetani. Shetani anautumia mwili wako kukushawishi utende dhambi. Hivyo ukiruhusu ..
Usiache kupaza sauti yako kama tarumbeta. Kuna watu wanasema kuhubiri injili masokoni na vijiweni ni kukosa kazi ya kufanya na kwamba watu wanaofanya hivyo hawapo sawa kiakili au ni wavivu wa kufanya kazi. Lakini wewe ambaye umeitwa kufanya kazi hii ya Mungu, nataka nikutie moyo kwa Neno la Mungu ya kuwa usiache kupaza sauti yako ..
TUONDOKEE HATUTAKI KUZIJUA NJIA ZAKO Ayubu 21:14 “Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako. 15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba? Hayo ndio maneno ya watu wengi waliofanikiwa katika mambo ya duniani, wakamsahau Mungu aliyewaumba. Lakini biblia inasema.. Ayubu 21:16 “Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao;..” Tena anasema.. “Maana ..
UKITII, YESU ATAKUOKOA. Ni Kwanini watakaotangulia kwenda mbinguni wawe ni watu wanaoonekana kuwa mbali na Mungu, kuliko watu wa kidini? Mathayo 21:31 “….Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.” Mpaka kupelekea Bwana Yesu kuzungumza maneno hayo, ni kutokana na mfano aliousema juu yake kidogo, uliowahusu watoto wawili wa ..
MIMI NDIMI NJIA, KWELI NA UZIMA. Yohana 14:4 “Nami niendako mwaijua njia. [5]Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? [6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”. Shalom karibu tujifunze Neno la uzima. Tukitaka kufika mahali Fulani au mji Fulani, ni wazi kuwa ..
KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE OUVU. Jina la Bwana wa Mabwana YESU KRISTO libarikiwe daima. Neno la Mungu linasema.. 2Timotheo 2:19 “Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE OUVU.” Kulitaja jina la Bwana ni zaidi ya kutamka kwa mdomo, ..
Jihadhari usipoteze nafasi ya kuingia mbinguni. (Sehemu ya pili) Kama Ukijifunza Biblia kwa undani utagundua kuwa Bwana Yesu hakuwa na wanafunzi 12 tu! Bali alikuwa na wanafunzi wengine wengi sana Zaidi ya 70 biblia inasema hivyo katika (Luka 10:1-2)…Lakini baadaye alikuja kuteua wanafunzi 12 tu miongoni mwao wakutembea naye kila mahali alikokwenda ambao aliwaita Mitume. ..