Elewa kwanini Damu ya Yesu Kristo inanena mema kuliko ya habili?

Maswali ya Biblia No Comments

Utukufu kwa Bwana Wetu Yesu Kristo,aliyetupa neema ya kutafakari Maneno yake ya uzima..

Yamkini umekuwa ukijiuliza sana kwanini maandiko yaseme damu ya Yesu Kristo inanena mema kuliko ile ya habili, na leo kwa Neema za Bwana tutaangazia..

Kama ni msomaji wa maandiko utakuwa unaelewa habari ya kaini na Ndugu yake habili, jinsi dhambi ya wivu ilivyomchukua kaini na kupelekea kumuua ndugu yake habili kwasababu walivyopeleka sadaka zao wote,ya kaini ilikataliwa na Mungu lakini ya habili i Mungu aliikubali, ndio sababu ya kumuua ndugu yake..

Embu tusome…

Mwanzo 4: 8 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.

9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10 Akasema, Umefanya nini? SAUTI YA DAMU YA NDUGU YAKO INANILILIA KUTOKA KATIKA ARDHI.

11,Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao”.

Jambo la kulizingatia hapo ni mstari wa kumi, Mungu anamwambia kaini sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka Katika ardhi, na hapa ajasema sauti ya “roho ya ndugu yako” bali ni damu ya ndugu yako, kumbe maana yake damu inazungumza, damu inaongea, damu inatoa sauti, na sauti yake haitoki mbinguni,bali kwenye ardhi,na hapa kuna uhusiano wa damu na ardhi,lazima ulifahamu hilo,ili uwe makini na uhai wa mtu,au damu,…

Ndo mana maandiko yanasema.. kwenye waebrania,

12: 24 inasema “Na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, INENAYO MEMA kuliko ile ya Habili”.

Umeona hapo, maandiko yanasema kuna damu nyingine,na hiyo damu nyingine inanena mema kuliko ile ya habili, na damu yenyewe si nyingine zaidi ya Bwana Yesu Kristo, haleluya, unapata wapi ujasiri wa kumkataa Yesu maisha mwako ndugu,

UTAJIULIZA DAMU YA YESU INANENAJE MEMA, KULIKO YA HABILI

Maandiko yametupa kuelewa habili alikuwa ni mtu wa namna gani kwa sehemu tunayoisoma kwenye maandiko, tunaona alikuwa mcha Mungu, mtu wa haki akimtolea Mungu sadaka zake kwenye sehemu zilizonona, alijitahidi kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwa kuzifuata sheria za Mungu, hivyo hata kifo chake kinatokea bado alikuwa katika haki yake ndo mana damu ilionekana bado kama ni damu isiyokuwa na hatia kwa kitendo cha kuuwawa na Ndugu yake, hivyo ikamfanya akiwa ardhini,au damu yake kushuka tu kwenye ardhi ikaanza kuzungumza..

zaidi ya yote, tunamwona pia na Bwana Yesu,yeye hakuwa na hatia yoyote ya kufa pale msalabani, sio kwamba dhambi zake na makosa yake ndio yaliyomfanya asulubiwe, sivyo, yeye hakuwa na dhambi wala kosa lolote, ndio maana maandiko yanasema,

Isaya 53:5

[5]Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,

Alichubuliwa kwa maovu yetu;

Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,

Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Umeona hapo, yeye hakuwa na hatia yoyote ya kufa kalvari.

Tusome tena..

Matendo 4: 25 “Nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?

26 Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.

27 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu YESU, ULIYEMTIA MAFUTA,”

Ukisoma zaidi utaona mwisho wa damu ya habili ilikuwa inanena hukumu juu ya ndugu yake, inanena kisasi, inanena ardhi ilaaniwe juu ya kaini, inanena mambo ambayo yanamtakia hukumu nduguye..

Lakini Damu ya YESU KRISTO,hiyo haikunena hukumu wala kisasi kwa wale waliomtendea mabaya, bali ilinena ondoleo la dhambi, ilinena msamaha, ndo mana Bwana akiwa pale msalabani alisema IMEKWISHA, tofauti na habili yeye hakuzungumza hayo, ndo mana kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwa na Yesu Kristo, kwasababu damu yake ilinena msamaha wa dhambi, damu inatupa sisi baraka zote na sio hukumu wala laana ambazo tulitakiwa tuzipate, hivyo tunasema damu ya Yesu Kristo inanena mema kuliko ya habili.

Hata sisi leo ikiwa tunatenda mambo maovu pamoja na wale wote walimtendea maovu kwa kumsulubisha Bwana msalabani tungestahili tupewe laana zaidi hata ile ya kaini, tungetakiwa tuwe tumeshakufa kwa kitendo cha kumwua mwana wa Mungu, Yesu Kristo, lakini kwa kuwa damu yake ilinena mema ndo mana mpaka leo tunaishi, tulitakiwa tupate laana, lakini ilituenenea baraka, zaidi tulitakiwa tuwe wote tumeshapotea kabisa lakini damu ya Bwana Yesu ilituenenea Uzima udumuo, Uzima wa milele, kupitia damu yake, Ni furaha iliyoje..

Ni damu iliyomwagika miaka elfu mbili iliyopita lakini mpaka sasa inanema mema, uzima hu ni kwasababu ya damu ya Yesu, mambo yanayoendelea kwenye hu ulimwengu ni kwasababu ya Damu yake, kubwa Katika yote, tumepata kibali cha kuzungumza na Mungu Mbinguni kwasababu ya damu yake Yesu,

Leo umeufahamu umuhimu wa damu ya Yesu Kristo kwenye maisha yako, kwanini bado unaendelea kumsulubisha, unamsulubisha kwa matendo yako mabaya, ni mwizi, unakunywa pombe, ni mzinifu, unazini mpaka na wanyama,unavaa nguo za ajabu, suruali, mshirikina,unajipodoa, kwa mawigi na hereni, na mengine mengi yanayofanana na hayo, lazima ujue kuna siku itafika hii damu haitanena mema bali hukumu kama ukiendelea kufanya dhambi..

Neno la Mungu linasema..

Waebrania 10: 26 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI;

27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

2, Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29 MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?

30 Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.

31 NI JAMBO LA KUTISHA KUANGUKA KATIKA MIKONO YA MUNGU ALIYE HAI.”

Umeona hapo ndugu yangu,usiidharau hii damu kipindi hiki inanena mazuri juu yako huku ukiendelea na kutenda dhambi,zaidi unatakiwa uogope sana, unavuta pumzi yake, kwasababu ya damu na huku unaenda kwa waganga, unalala unaamka unaenda kunywa pombe,ni damu yake, lakini ipo siku hukumu itakuja juu yako kwa mambo yako mabaya unayoyafanya..na hakutakuwa na msamaha tena,

Kwanini hayo yakukute ndugu, amua kumkabidhi Yesu Kristo maisha yako leo, ni yeye aliyekufa kwa ajili yako akasema,imekwisha, ni yeye anayekupa hiyo pumzi unaivuta bure bila malipo yoyote,ni yeye Yesu Kristo, ni wakati wako sasa, damu yake inakunenea utubu kwa kumaanisha kabisa na kisha ukabatiwze kwa jina lake Yesu Kristo,sawa na matendo ya mitume 2:38-39, upokee Roho Mtakatifu atakayekuongoza.. unasubiri nini..

Shalom, Maran atha..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *