elewa maana ya ufunuo 20:13, bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake

Maswali ya Biblia No Comments

 

Tusome…

Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

13 BAHARI IKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE; NA MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.

 JIBU,

Kipindi cha mwisho kabisa kutakuwa na hukumu, na hukumu hiyo inajulikana Kama hukumu ya kiti cheupe cha Mwanakondoo.. hukumu hii inajumuisha wafu wote waliopo katika makaburini, hii ni mbali na watakatifu,

hukumu hii haitachagua wakubwa Wala wadogo, wazee au vijana, wote walio waovu watafufuliwa na kila mmoja atasimama mbele za Bwana na kuhukumiwa sawa na matendo yake yalivyo na kutupwa kwenye ziwa la moto na kuangamia milele..

Maandiko yanatupa kuona ,siku hiyo waovu watatokea sehemu mbili..

1, ya kwanza, ni baharini

2, na ya pili ni Mauti na Kuzimu

Fahamu lugha iliyotumika hapo ni lugha ya kinabii kwasababu hakuna uhalisia kuwa bahari inayo wafu wake, sivyo..

Je bahari kuwatoa wafu wake,ilimaanisha nini

Lazima tufahamu siku zote bahari ni kubwa, haina mwisho wake, kana kwamba ukipotea huko ni kama umepote moja kwa moja, na kulingana na biblia, bahari au maji mengi inawakilisha ni ulimwengu,

Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha

Hii ina maanisha Katika siku ile ya mwisho, wafu wote kutoka mataifa yote duniani waliokufa kuanzia kipindi cha Adam hadi kipindi cha Bwana Yesu kurudi kulichukua kanisa lake, sasa wote hao wote watakuwa ni wafu watokao baharini (ulimwengu) ndipo watafufuliwa na kuhukumiwa..

Mauti na kuzimu kulifunua nini?

Na kama tunavyofahamu baada ya unyakuo kupita tukio litakalofuata ni dhiki kuu, kipindi hiki kinafahamika kama ni utawala wa shetani(mpinga Kristo) kupitia dhiki hii watu wengi sana watauliwa kwa kuwa ni dhiki ambayo Mungu ameiruhusu kwa shetani kwa watu waovu wote duniani, na wote watakaoikataa chapa, watauwawa..

Soma ufunuo 6:8

Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda JINA LAKE NI MAUTI, NA KUZIMU AKAFUATANA NAYE. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi”.

Umeona hapo, maandiko yamemtaja huyo farasi wa kijivujivu kwa jina la mauti akiwa sambamba na kuzimu, ibilisi akifanya kazi yake wakati huo, atafanya vifo vya watu kufikia robo  waliopo katika dunia, kwa hesabu ya haraka ni watu bilioni mbili watauwawa, na hapo itakuwa ni ghadhabu ya Mungu, vita ya harmagedoni, magonjwa, sasa watakaokufa hapa wote watakuwa chini ya mauti na kuzimu..

Utakuwa umeshapata uelewa biblia inapozungumzia mauti na kuzimu ikawatoa wafu wake, kuwa ni wafu waliokufa katika kipindi cha dhiki kuu, ambao waliokuwa chini ya mpanda farasi wa nne aliyejulikana kama mauti na kuzimu..

Utajiuliza kwanini maeneo yote yatajwe?

Hii inatuonyesha au kutupa kujua kuwa,katika hukumu hatabaki mfu yoyote, hii itakuwa ni hukumu ya ulimwengu wote kwa ambao hajaenda kwenye unyao, au hawajaikataa chapa ya mnyama..

Umekufa katika uovu wako, umekufa ukiwa mzinzi, mwizi, mtukanaji, mwongo sehemu yako utakayokwenda utakwenda kwenye bahari ya kiroho, lakini ukifa kwenye dhiki kuu Moja kwa moja utakwenda kwenye mauti na kuzimu na wote kwa pamoja mtafufufuliwa na kutolewa hukumu kila mmoj kwa kipimo chake na kisha kutupwa kwenye ziwa la moto.

Unayesoma Maneno haya, fahamu hukumu ya Mungu mwenyezi ni ya kuogopa sana, kwasababu hakuna nafasi ya pili utakayopata baada ya kifo, ukiondoka gafla ni Moja kwa moja jehanamu ukiteseka mpka ukingoja ufufuo ufike, waliopo huko wanalia kwa majuto makubwa wakitamani hata sekunde moja watubu lakini haiwezekani..

Tubu leo kwa kumaanisha,mpokee Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako, unyakuo ni wakati wowote..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *