Elewaa maana ya 2Petro 2:13 wakidhani kuwa ulevi wakati wa mchana.

Maswali ya Biblia No Comments

Hebu tuvipitie vifungu vyenyewe

2Petro 2:12 “Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, WAKIDHANIA KUWA ULEVI WAKATI WA MCHANA NI ANASA; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi”;

Hivyo tunaona Mtumishi wa Bwana Petro, alikuwa anafafanua kuwa watu waovu wanavyoelekea katika shauku na tamaa za mwili, ukianzia kusoma mstari wa juu utaona akiwalinganisha na watu wa Sodoma na Gomora..Na moja ya mambo yao ndio hayo aliyotuambia ni “Wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa” akiwa na maana kuwa, wamefikia kiwango ambacho wao anasa zao kama ulevi hawazifanyi tena usiku, bali hata mchana.

Inajulikana kuwa anasa zote zinafanyika wakati usiku.. Na ndio maana wakati ule wa Pentekoste, Roho aliposhuka, wale watu waliwashutumu mitume kuwa wamelewa kwa mvinyo, Lakini Petro aliwaaambia, hakuna aliyelewa, kwasababu sasa hivi ni saa tatu ya mchana (akiwa na maana ni saa 9 alasiri), hakuna mtu anayelewa muda huo.

Matendo 2:13 “Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.

14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya
mchana”;

Soma pia andiko hili

1Wathesalonike 5:7 “Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku

Kama tulivyo soma, hivyo mpaka mtu imetokea anafanya anasa kama hii ya ulevi wakati wa mchana,. Ni mtu aliyevuka viwango, haoni tena haya kufanya mambo yake maovu hadharani amewazidi hata  wenye dhambi wengine wafanyao mambo kama hayo.Ndivyo walivyokuwa watu wa Sodoma na Gomora, walivuka mipaka waliufanya ushoga wao kweupe kabisa, bila haya wala aibu yoyote.

Ni kama tunavyoona hakuna kificho tena duniani, mambo ya gizani yanafanyika wazi kwenye matamasha, kwenye TV, yanatumwa Whatsapp, yanaonekana Youtube na kwenye mitaa yetu.

Sasa ni kutukumbusha kuwa tunaishi katika nyakati za mwisho za kurudi kwa pili kwake Yesu Kristo. Wakati huu ni wa kuilinda mioyo yetu isielemewe na mambo ya ulimwengu huu, kama alivyofanya Lutu alivyokuwa Sodoma. Kwasababu ulimwengu huu utakwenda kuangamizwa kwa moto muda si mrefu, kama mtume Petro alivyomalizia kusoma katika waraka huo.

2Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?”

Je umeokoka? Je parapanda ikilia leo unaouhakika wa kwenda mbinguni?. Majibu sote tunayo. Mwennendo wako katika Ukristo ndio unaodhihirisha wewe unakwenda wapi baada ya maisha haya tuwe makini sana ni siku za Mwisho hizi.

Bwana anakuja

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *