Fahamu maana ya Kimiami

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo Mwokozi wetu.

Kimiami kwa lugha ya sasa ni dirisha kubwa lililo katika ghorofa. Katika lugha/Kiswahili cha zamani ilimaniisha hivyo.

Sasa ukisoma katika biblia ya kiingereza inaeleza wazi wazi kabisa maana yake ni nini!!

Song of Solomon 2:9
[9]My beloved is like a gazelle or a young hart. Behold, he stands behind the wall of our house, he looks in through the WINDOWS, he glances through the lattice.

hii imeweka bayana kabisa ni nini maana yake sasa tunaporudi kusoma katika lugha ya Kiswahili ndio kidogo inaleta msamkati kwa sisi watu wa sasa.

Wimbo 2:9 “Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu, Achungulia dirishani, atazama kimiani”.

Hivyo kimiami ni dirisha kubwa lililo katika ghorofa juu!

Mfano wa madirisha hayo moja wapo ni lile aliloanguka Eutiko

Matendo ya Mitume 20
9 Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika.

10Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.

Alikuwa ameketi ghorofa ya tatu katika dirisha kubwa au tunaweza kusema KIMIAMI.

Na mfano mwingine ni dirisha lile aliloanguka Mfalme Ahazia akaugua sana karibu na kufa na akamlilia Bwana.

2Wafalme 1:2 “Na Ahazia AKAANGUKA KATIKA DIRISHA la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu”.

Hivyo kimiani ni dirisha kubwa juu ya ghorofa!.

Ubarikiwe sana na Bwana YESU.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *