FAHAMU MAANA YA MITHALI 29:25.

Maswali ya Biblia No Comments

FAHAMU MAANA YA MITHALI 29:25.

Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo. 

Maandiko yanasema..

Mithali 29:25”Kuwaogopa wanadamu huleta mtego;Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.”

Je kuwaogopa wanadamu kunaletaje mtego? Na ni mtego gani huo unaweza ukampata mtu kama akiwaogopa wanadamu?

Mambo mengi yanayafanya watu kwa hofu ya kuwaogopa watu wanaowazunguka. Na kuwahofu kuwa itakuwaje nisipofanya hivi na vile? Wanajikuta wanafanya mambo yanayomchukiza Bwana kwa kufanya mambo fulani kwa hofu ya kuwaogopa watu..

Kama hofu watu watakuonaje ukiamua leo hii kumpa maisha yako Yesu Kristo maisha yako, watu watakuonaje ukiacha mambo ya kidunia na kuamua kugeuka kuacha kupaka lipstick,kuvaa suruali,vimini,kusikiliza miziki ya kidunia nk.

Tutaangalia mifano ya watu wachache waliofanya makosa kwa kuwaogopa tu wanadamu.

1.Herode.

Herode alimuuwa Yohana Mbatizaji ili kumpendeza mke wake na binti yake. Ukisoma Marko 6:21-27 tutasoma mistari micheche kulithibisha hilo..

Marko 625 Mara akaingia kwa haraka mbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.

26 Mfalme akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia.

27Mara mfalme akatuma askari, akaamuru kuleta kichwa chake. Basi akaenda, akamkata kichwa mle gerezani,

28 akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye.

Unaona hapo kwenye mstari wa 26? Alijikuta anafanya vile kwa sababu ya kuwaogopa watu waliokuwa wameketi chakulani ijapo hakupenda lakini alifanya vile kuwalizisha mke na binti yake kwa hofu ya wale watu pia waliokuwa wamekaa chakulani.

2.Sauli.

Mfalme Sauli nae alipoteza ufalme wake kwa kukiuka amri ya Bwana aliokuwa amemuagiza kuwa atakapokwenda kule akauwe kila kitu lakini hakufanya hivyo kwa kumuacha mfalme Agagi hai badala ya kumuua kwa kuwaogopa watu wale na ufalme wake akapewa Daudi.

1 Samweli 15:24 ““Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya Bwana, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao.

Unaona aliwaogopa wale akatii sauti yao na hiyo yalikuwa ni machukizo kwa Bwana.

3.Haruni.

Haruni pia wana wa Israeli walikuwa wanataka kumuuwa pale walipomtaka awatengenezee ndama wa dhahabu ili wamuabudu. Soma Kutoka 32:22-24.

Lakini kinyume chake wako watu ambao walikuwa tayari kufa lakini tumaini lao walikuwa wameliweka kwa Mungu hawakuwaogopa na kuwatii wanadamu.

Meshaki,Shadraka na Abednego walimtumaini Bwana walipokataa kuisujudia sanamu ya Nebukadreza hata kutupwa katika Tanuru ya moto na wakawa Salama kabisa kwa Bwana kuwaokoa na kuwatoa humo salama.

Danieli pia alimtumaini Bwana hata akawa Tayari kutupwa kwenye tundu la simba na akatoka mle akiwa salama kabisa. Ni kwa sababu hakukubali kuwatii wanadamu kwa kumkataza asifanye ushirika na Mungu kwa kufanya ibada.

Hivyo pia ili na sisi ili tuweze kuwa salama hatuna budi kuutafuta utukufu utokao kwa Mungu na si kwa mwanadamu kwa kuamua kumtii Yesu Kristo na kupita katika njia yake haijalishi dunia nzima itatukataa na kutuona hatufai tujikane nafasi kwa kuamua kumfata kweli Yesu Kristo Bwana wetu.

Yohana 5:44

[44]Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?

Hivyo tumaini letu liwe kwa Yesu Kristo hata kama tunaona hakuna namna ya sisi kuwa salama tunatengwa na kufukuzwa bado tuendelee kumtazama yeye peke yake naye hatatuacha kamwe kama maandiko yanavyosema katika..

Zaburi 125:1“Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.”

Kama hujamwamini Yesu Kristo muamini leo upate ondoleo la Dhambi na upate uzima wa milele. 

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *