NINI MAANA YA MITHALI 29:5

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo. 

Je? Mtu mwenye kujipendekeza ni mtu wa namna gani?

Mithali 29:5Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake’.

Kabla kwenda kuutazama vizuri mstari huu ni vizuri tufahamu nini maana ya kujipendekeza?

Kujipendekeza. Ni kitendo cha mtu kumsifia mtu mwingine kwa sifa nyingi ambazo zingine hakustahili kuwa nazo au hana kabisa.

Kwa kumzungumzia mema peke yake pasipo kumkosoa wala kumwambia ukweli asilimia kubwa ya watu wanaojipendekeza ni watu wanaosema uongo tu kwa lengo la kupata kitu fulani kwa ajili ya manufaa yao wenyewe tu. Na mtu anaejipendekeza anaeleza mabaya ya watu wengine kwa huyo mtu nk ili wengine waonekane hawafai ila yeye ndio anafaa.

Sasa kujipendekeza ni jambo baya na lisilompendeza Bwana kabisa maana lina madhara mkubwa sana hasa kwa yule mtu anaefanyiwa kitendo hicho maana ni jambo litakalomuangamiza kabisa.

Ndio maana maandiko yanasema..”unamtandikia wavu ili kuitega miguu yake”.

Hili jambo ni kweli kabisa leo hii viongozi wengi wa nchi jambo hili limewagharimu kwa sehemu kubwa sana hata kuiharibu nchi pengine wanakuwa ni wauwaji kabisa na wakatili wa kupindukia kwa sababu tu ya wao kuwa na uchu wa madaraka kutokana na sifa za uongo wanazopewa na watu wanaojipendekeza kwao.

Mfano kama huo tunaona hata kwa Mfalme Sedekia kwa wale manabii waliojipendekeza kwake kwa kusema uongo kuwa hakuna baya lolote litatokea lakini Yeremia alimwambia ukweli na hawakutaka kumsikiliza kabisa na mwisho wa siku Sedekia anatobolewa macho kwa sababu hiyo hiyo..

Vivyo hivyo hata Mfalme Ahabu kwa wale manabii mianne wa uongo waliomdanganya matokeo yake akaenda vitani na akapigwa mshale uliopelekea mauti yake baada ya kuacha kumsikiliza Mikaya nabii.

Ni jambo gani tunajifunza katika hili jambo?

Hii pia inatufundisha kama watu tuliomwamini Yesu Kristo iwe ni makazini kwetu tusiwe watu wa kujipendekeza kwa mabos zetu kwa kuwapa sifa wasizokuwa nazo na kuyasema mambo ya wengine ili tupendwe tuepuke kabisa.

Maana lengo kubwa si kumsaidia huyo mtu bali ni kumuangamiza kabisa mtu ambe tunajipendekeza kwake. Hapo unakuwa unamtandikia wavu mbaya sana na mwisho wa siku utamuangamiza..

Je utapata faida gani kumuangamiza mwezako kwa tamaa ta matakwa yako kutimia yeye anakwenda kuzimu ili wewe ufaidike na vitu vya kitambo tu! Acha kabisa kama umeanza kuwa na tabia hiyo tubu kuanzia sasa(Geuka) 

Hivyo ikiwa kuna mahali kweli anastahili pongezi/sifa na niza kweli basi mpongeze ikiwa anastahili kukosolewa hata kama ni boss wako fanya hivyo wala hatakufukuza kazi. Kumbuka wewe ni Nuru ya ulimwengu kamwe usichangamane na giza kabisa.

Ubarikiwe sana..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *