Uchawi ni jambo lolote linalofanyika nje na nguvu za Mungu, kwa sababu hakuna nguvu nyingine inayofanyika nje na nguvu za Mungu zaidi ya shetani..
Na uchawi umebeba mambo mengi, baadhi yake ni kuloga, kuagua, kutazama utabiri wa nyota, kubashiri, kusihiri, kuabudu sanamu, mambo haya huwaaminisha watu kuwa wanaweza kupata msaada tofaututi na nguvu za Mungu
Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.’’
Uchawi ni jambo ambalo Mungu analichukia sana, ndiyo maana tunaona alianza kulionya lisifanyike tangu kipindi cha Israeli kutoka misri kwenda kaanani, maana ilikuwa mtu anayekwenda na agizo Hilo adhabu yake ilikuwa kifo (kutoka 22:18)
Ukisoma pia
Ufunuo 22:14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya
Uchawi ni chukizo kubwa sana mbele za Mungu, pia uchawi si ule tu wa watu wanaopaa na ungo bali mtu yeyote anayeshiriki hata kwa kwenda kwa huyo mganga tayari ni wewe ni mmoja wapo wa wachawi, kuamini kuwa ukiweka zindiko utakuwa salama, au kutazama nani anayekuchezea nk hapo ni sawa na kuwa miongoni mwa wachawi wabobezi
Kama ulikuwa ulijui hili na bado, ujampokea Yesu maishani mwako wakati ni sasa, maana mambo unayofanya ni mabaya mbele za Mungu wala hayamfurahishi tubu Leo ili uwe salama.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.