Shalom karibu tena katika kujinza neno la Mungu
Wagalatia 2:3 “Lakini Tito aliyekuwa pamoja nami, naye ni Myunani, hakulazimishwa kutahiriwa.
4 BALI KWA AJILI YA NDUGU ZA UONGO WALIOINGIZWA KWA SIRI; AMBAO WALIINGIA KWA SIRI ILI KUUPELELEZA UHURU WETU TULIO NAO KATIKA KRISTO YESU, ILI WATUTIE UTUMWANI;
5 ambao hata saa moja hatukujitia chini yao, ili kwamba kweli ya Injili ikae pamoja nanyi.”
Tutatazama je ni uhuru gani ambao waliomwamini Yesu Kristo wanakuwa nao, uhuru ambao tuliopewa sisi ni uhuru ambao tumeondolewa katikati utumwa wa sheria fulani, mfano kushika sabato, kutokula baadhi ya vyakula mfano, nguruwe, sungura samaki asiye na mapezi nk…. Sasa mambo hayo yote tumeshakuwa huru nayo, utumwa wote Yesu Kristo aliuondoa pale kalvari
Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo
Mtume Paulo aliandika waraka huu, kwa sababu aliona wayahudi waliojiingiza kwa Siri ili kuupeleleza uhuru walikuwa nao walilo mwamini Yesu, na lengo halikuwa katika kumtumikia Mungu bali walienda kwa kusudi la kuwaondolea ule uhuru waliokabidhiwa na Yesu, kwa kuwa tia katika mwenendo wao na kuwapa kushika mambo ambayo hata wao hawakuweza kuyafanya, kwa kuwarudisha katika sheria ambayo tayari wapo huru nayo
Jambo hili linatukumbusha, nasi katika kipindi hiki ambacho tupo wapo pia watu, au watumishi ambao lengo lao si kumtumikia Mungu ila tu ni kwa ajili ya kuondoa ule uhuru ambao tayari wameshakwisha ufahamu, na kuleta mapokeo ambayo yapo kinyume na neno la Mungu
Sasa huko ndiko kuupeleleza uhuru ambao tumepewa na Kristo… Kwa lengo la kumwondoa mtu katika Imani yake
Ni wakati wa kuwa macho ili tuweze kupambanua Roho hizi ili zisitutoe katika njia Bora ya Mungu..
Ubarikiwe
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.