Nakusalimu kupitia jina la Mwokozi
Hili limekuwa swali kwa kila mwamini, kwanini tunatubu kila siku, na wakati Kristo mwokozi wetu alizibeba dhambi zetu zote,
Tusome
1Petro 2:24 “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa”.
Ni kweli Yesu Kristo alizichukua dhambi tena, lakini siyo kwamba tayari tumekamilika katika yote, kumbuka hii miwili tuliyopewa ni dhaifu, ndiyo maana tukapewa nguvu ya kuushinda, hivyo kuna baadhi ya vikasoro vinakuwepo tu si kwamba mtu atapenda kuvifanya lakini vinatokea tu unashangaa mtu kafanya, mfano kuwaza vibaya sasa haya Moja kwa moja ni mapambano na yapo ili tuweze kuufikia ule ukamilifu ndiyo maana baada ya mtu kutambua kuwa amekosea hutubu
Ndiyo maana Bwana Yesu alitufundisha kuomba hivi
Luka 11:1 “Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
4 UTUSAMEHE DHAMBI ZETU, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu]”.
Swala la kutubu haimaaanishi Yesu hakukamilisha pale msalani, Bwana alikamisha mambo, mwanadamu kutubu ni kuonyesha unyenyekevu mbele za Mungu, maana kuna makosa tunayafanya kwa kujua na wakati mwingine pasipo kujua sasa hayo yote tukiyajua moja kwa moja, kinachofuta ni toba kwa BABA YETU.
Lakini kama tunavyojua ile siku ya mwisho tutaondolewa miili hii na tutavikwa miwili mipya ambayo ni mikamilifu , hivyo hichi ni kipindi cha kutengeneza unapoona kuna jambo halipo sawa nenda mbele za Mungu
Waefeso 4:30
[30]Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
Ubarikiwe .
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.