Jina la Bwana libarikiwe karibu tuweze kujifunza tena Neno la Mungu litupalo uzima ndani yetu…
Tusome andiko hilo ili tupate maana ya mstari huo
Zaburi 38:10 “Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka”.
Maana ya neno “moyo wangu unapwita pwita, ni sawa na kusema moyo wangu unauma hivyo maana ya kupwita pwita ni moyo kuuma au kwenda mbio.
Hapa mwandishi wa zaburi alikuwa anaonyesha hali au kipindi alichokuwa anapitia kwa wakati huo hadi ikamleta maumivu makubwa katika moyo wake, ndipo hapo aliposema “Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka”.
Ukiendelea mistari ya mbele amejielezea zaidi ni kitu gani anapitia
Zaburi 38:11-12
[11]Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo languNaam, karibu zangu wamesimama mbali.
[12]Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego;
Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa.
Mara nyingi mtu yeyote anayepitia kipindi fulani kigumu, kinachosababishwa na watu fulani hupelekea moyo kuuma au kusikia uchungu, kutokana na hizo hali, lakini katika yote hayo yote Neno la Mungu linatuelekeza. hata upitie hayo yote wewe kuwa waombaji, msomaji wa neno, nk. Katika jumla ya yote unapopitia hali kama hizi isikufanye ukawa mbali na Mungu bali zidi kujisongeza kwake maana kwake tunapata jawabu la kila jambo na faraja na amani
Zaburi 40:1-5
1 Nalimngoja BWANA kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi;
Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini BWANA
4 Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.
5 Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki.
Mtegemee Mungu katika yote
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.