Fahamu namna gani ya kuwaombea Watoto

Watoto No Comments

Jina Bwana Yesu libarikiwe milele, karibu tujifunze Neno lake..

hili ni fundisho maalumu linalomuhusu mzazi au mlezi, kama upo kwenye nafasi yoyote ya kulea basi zingatia haya,

Kitu pekee na kikubwa na cha kuzingatia wewe uliye Katika nafasi ya ulezi ni MAOMBI,

Maombi ni silaha kubwa inayoweza kuangamiza mishale yote ya adui shetani, na Maombi ni ya kila siku,sio siku moja, tunaomba kila siku kwasababu mshitaki wetu naye anawafuata kila siku watoto ili awameze na kwa kuwa anajua imendikwa uzao wako utamponda yeye kichwa, soma (mwanzo 3:15)

Yapo mambo mengi unaweza kuyaomba kwa mwanao lakini leo kwa Neema zake tutaangalia ni Vipengele gani unaweza kuviombea kwa Watoto wako,

1, OMBEA WOKOVU

Omba Neema ya wokovu kwa Watoto wako, kwamba wamjue Mungu hata wakiwa Katika kipindi hicho cha udogo, haijalishi una mimba bado, wewe mnenee Mtoto wako wokovu ili atakapozaliwa aanze kutembea na Mungu,

Simama na neno hili kwenye maandiko ukimsihi Bwana,omba kwa imani kabisa na kwa kumaanisha kwamba unataka watoto wako wapate wokovu ili wamtumikie Mungu..

1 Timotheo 3:15 “na ya kuwa TANGU UTOTO umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu”

2, OMBEA UTII NA HESHIMA

Hili ni jukumu lako mlezi la kumuombea Mtoto awe na utii ndani yake,na heshima itawale bila ubaguzi, Watoto wengi hawana haya, wengine wamekumbwa na pepo la kiburi, hawana utii ndani yao, hivyo utakapozidisha kumuombea na kuonyesha badiliko ndivyo watakavyozidi kuongeza heri za miaka mingi ya kuishi..

Waefeso 6:1 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,

3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”.

Wakati wa kuomba kwako simama na vifungu hivi vya kimaandiko, ni Katika kumsihi Bwana Katika Neno lake..

3, OMBEA ULINZI

Adui shetani ni mharibifu hata kwa watoto wadogo, maandiko yamemtaja kama mharibifu na muuwaji, hivyo huna budi kuwaombea ulinzi wa ki-Mungu uwe pamoja nao, ulinzi kwenye afya zao, maisha yao ya kiroho mwenendo wao wa tabia ili adui asipate kuwavuruga au kuwaundia tabia mbaya..

Msihi Bwana kwa andiko lake..

1Yohana 5:21 “Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu”

4, OMBEA UKUAJI WA KIROHO NA KIMWILI

Msingi mwingine mkuu ni kuwaombea ukuaji wa kiroho, kwamba waendelee Mbele Katika Imani, wsiyumbishwe bali wazidi kumjua Mungu na kumtumikia yeye siku zote, ombea maendeleo hayo ya rohoni, zaidi ukiwaombea afya zao, njia zao sizikatishwe kwa magonjwa au chochote kibaya..

Luka 2:39 “Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.

40 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake”.

5, OMBEA ELIMU YAO

zidisha Maombi yako kwa watoto wako ili wazidi kuwa na akili Katika elimu yao ya shuleni, pale wanapojifunza au kufundishwa basi wakawe na ufahamu wa haraka wa kuelewa, ili wawe kichwa na sio mkia,

  4:13 “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako”

6, OMBEA WAJAZWE ROHO MTAKATIFU

Likumbuke hili kila siku, kuwaombea ujazo wa Roho Mtakatifu ili Neema ya Mungu izidi kuongezeka juu yao, nafasi ya Roho Mtakatifu ni kubwa sana kwa mtoto wako maana ndiye atakayekuongoza, kama Yohana mbatizaji alivyopokea Roho Mtakatifu akiwa tumboni na wewe huna budi kumuombea mwanao hata kama ni mchanga kiasi gani, omba,omba,ajazwe Roho..

Matendo 2:38 “ Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Kuwa na desturi ya kuwaombea wanao, kila siku, jiwekee na ratiba kabisa itakayokusaidia kuwaombea kwa mambo hayo, na ukiwa mwaminifu hapo basi utaona badiliko kubwa kwa watoto wako, haijalishi alikuwa mtundu,au asikii kiasi gani, kazi ya kutengeneza ni ya Bwana Yesu, wewe omba sana, funga na kuzidi kujitoa kwa mali zako ili kuonyesha msisitizo Mbele za Mungu..

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *